Humu ndani kuna watu wana roho mbaya

Humu ndani kuna watu wana roho mbaya

Hakuna sehem watu wana roho nzuri kama hapa JF....ni wakarimu sijapata ona,,...ila kwa kauli yako hiyo,,....sidhan kama watakusaidia,,.... em waombe radhi kwanza na ujifunze kuongea vizur na watu
 
samahani nimekosea wapi?

Umekosea pale ulipoanza na kichwa cha habari.......humu ndani kuna watu wana roho mbaya sana.......hapo unategemea kupata msaada wetu kweli........?
 
saa me ntafanyaje kaka nimeomba msaada toka mwezi wa nne nilienda kwa mkuu wa wilaya wakanijibu vibaya sasa mimi nifanyeje jaman
 
saa me ntafanyaje kaka nimeomba msaada toka mwezi wa nne nilienda kwa mkuu wa wilaya wakanijibu vibaya sasa mimi nifanyeje jaman

Sasa huyo mkuu wa Wilaya ndio Jamii Forums.....?
 
Tembea mbele huko, jisaidie mwenyewe, watu ndio wanavyoomba msaada namna hiyo.
 
samahani kaka nimechanganyikiwa kuona vijana wengine wanapelekwa shule mimi sina pakuanzia
 
haya bwana hata kijana wako hatafanyiwa hivi ipo siku haujui moyon naumia kiasi gani...
 
haya bwana hata kijana wako hatafanyiwa hivi ipo siku haujui moyon naumia kiasi gani...

Kijana sikiliza.......humu ndani hata rais wako yupo na waziri wa hiyo elimu yako.......sasa ukiomba kibabe namna hii......unaonyesha huna nidhamu......kijana msomi anatakiwa awe na nidhamu.........ukisoma ukipata uongozi wewe si utakata watu vichwa.....? Kuwa mtulivu omba kwa adabu.......kusaidiwa kwako JF inawezekana sana.......
 
Ndivyo ulivyofundishwa kuomba hivyo? Hayo malezi uliyopata kiboko! Napata picha ndugu yangu anakuja kwangu anaanza na hiyo statement yako 'una roho mbaya, si unisomeshe?'

Unless wewe ni mkenya. Manake ndo tumezoea unasrma 'aki weeh ni mchung, si unipatie doo nikanunue credoo niweke kwa simu nipigie sista angu?'

Cc Highlander

he, mbona sijaielewa hii. hizo doo za credoo zinanyesha wapi kama mvua tupeane japo taarifa fupifupi jamani
 
Last edited by a moderator:
saa me ntafanyaje kaka nimeomba msaada toka mwezi wa nne nilienda kwa mkuu wa wilaya wakanijibu vibaya sasa mimi nifanyeje jaman

sijui kwa nini vijana wa siku hizi hatuna uvumilivu,watu wamesumbuka kutafuta scholarship miaka mingi,lakini ungwana wao na uvumilivu walikuja fanikiwa
kwanza mi ndio naona ombi lako hilo leo, sio kila mwana jf alipata kuona ombi lako tangu mwezi wa4,kumbuka kuna waliojiunga jf mwezi5,6.
1 kwanza omba usaidiwe kuedit iyo heading yako
2 jaribu kuwa mvumilivu kwenye maisha
3 usiwe mtu wa kujiliza jiliza

nb kuna mdau apo juu amekwambia humu jf kuna kila aina ya watu,rais,mawaziri, wabunge,wakurungezi wa taasis kubwa,wanafunzi,wafanyabiashara,raia wa kawaida etc
 
Back
Top Bottom