Huna baya MK14 Meddie Kagere

Huna baya MK14 Meddie Kagere

Aisee wewe akili yako ni fupi mno tunaupimaje ukali wa striker?
Usianze matusi sasa jadili tu mada. Ukianza matusi nitakudhalilisha maana naamini siwezi kuwa na akili fupi zaidi ya mama yako.
Striker anapimwaje zaidi ya record ya ufungaji na consistency?
 
Medieeee kagere MK14 kifaru cha kinyarwanda (in Nurdin Suleyman voice)
Aah striker asiye na mbamba kabisa
 
Ma Foward wa Bongo wana kuaga wa MOTO sana wakiwa hizi Team kubwakubwa tu wakienda hizi Team Ndogo wanapotea unaanza kujiuliza ule uwezo umepoteaje?

Hapo unagundua huenda ni kweli hizi Team Kubwa hua zinahonga Mabeki wa Vitimu vidogo vidogo ili foward zao zifunge zionekane za Moto.

Hivi Kweli Mbappe atoke Leo PSG aende Nantes atamaliza Msimu na Goli 3 na Kukosa Penalty Kipumbavu?

Afadhali ingekua amehama Ligi yani ndani ya Ligi ileile aliyoiteka Miaka 5+?

KAGERE ALIKUA MZURI..Ila hio Hoja Niliyoibua izingatiwe!
Hebu nikumbushe vizuri, Fernando Torres alivyohama Liverpool kwenda Chelsea, form yake ilikuwaje? Au Alexis Sanchez alivyotoka Arsenal kwenda Man UTD, kiwango chake kilikuwaje?

Kagere aliachwa na Simba baada ya kiwango chake kuanza kushuka, vingine wasingemuachia. Sasa kule alikoenda, angalia wachezaji wanaomlisha then Rudi angalia umri wake, hapo utaona kwamba kutofunga kwake kunasababishwa na mengi.

Kusema vilabu vikubwa vinahonga mabeki wa timu ndogo, hiyo ni nadharia tu. Kama timu zinahonga ili washambuliaji wake wafungwe, basi mpaka Leo Sarpong na Yikpe bado wangekuwa Yanga
 
Kama kumewahi kuwa na Striker wa kigeni hatari kama Kagere nikumbushwe. Hakuna cha kusubiri azoee ligi wala nini. Halafu jitu la kazi halina shobo na media wala ulimbukeni wa kulewa sifa
Sio kweli, unamjua Jama MBA wewe au Mlete Mzungu? Walikuwepo wengi wazuri toka enzi za akina Nonda mkuu, walikuwa wazuri japo hawajafunga goli nyingi kama MK14.
 
Mimi shabiki wa Yanga,kimpira sijawahi kupenda aina ya style ya kagere vile anavizia muda wote,but sijawahi kupinga umahiri wake wa kucheza na nyavu
Siku moja tupo na washikaji tunacheki game ya Simba na Namungo kwa mkapa,dk 90 ngoma 0-0 ,nikajua mtani kapoteza points,ghafla yakamwaga maji na hajib au tshabalala Mpira wa chini kagere kapiga kichwa,goooooooal...ghafla nikastuka nimesimama napiga makofi karibu 20 seconds,nilishangia goal,sio ushindi wa Kolo
 
Mimi shabiki wa Yanga,kimpira sijawahi kupenda aina ya style ya kagere vile anavizia muda wote,but sijawahi kupinga umahiri wake wa kucheza na nyavu
Siku moja tupo na washikaji tunacheki game ya Simba na Namungo kwa mkapa,dk 90 ngoma 0-0 ,nikajua mtani kapoteza points,ghafla yakamwaga maji na hajib au tshabalala Mpira wa chini kagere kapiga kichwa,goooooooal...ghafla nikastuka nimesimama napiga makofi karibu 20 seconds,nilishangia goal,sio ushindi wa Kolo

View: https://youtu.be/fddY9bgDBMo?si=Qigxv3o7wcyf1I8L
Kula chuma hicho Mtopolo. Ndio maana kikaitwa kifaru
 

View: https://youtu.be/fddY9bgDBMo?si=Qigxv3o7wcyf1I8L
Kula chuma hicho Mtopolo. Ndio maana kikaitwa kifaru

Haha Safi Sana ndugu kumbe bado nna kumbukumbu,Mali imetoka kwa ajib, Mohammed Katia majalo...

Kagere bado mtu but wengi hawawezi kucheza kwa nguvu bila pressure,wewe fikiria why Simba&Yanga zinasajili wachezaji wa kawaida ambao hata national teams wanazotoka hawaitwi,but wakifika bongo kelele za mashabiki, pressure ya matokeo ,msukumo wa viongozi vinafanya wajitume Sana wazidi kua Bora ,viwango vinapanda wanaitwa kwao...mfano Mayele,inonga,Diarra chama,musonda hawakua Bora walipotoka Kama walivyo Sasa.,
 
Huyu alikuwa mwamba kweli kwenye ubora wake siyo poa..
 
Prince Dube sema tu yuko Azam
Binafsi sikuwahi kuwa na shaka na Meddie Kagere kwa sababu moja kuu, Mk14 alikuwa akitumia natural power mara kadhaa amekuwa akijua kazi yake ya kujiweka kwenye position! Namfananisha na Chicharito enzi zake akiwa Man U! Yaani pasi inapigwa unakutana na Kagere! Safi sana.
 
Back
Top Bottom