....Hunenepa sana baada ya kujifungua!

Chakula kinaongezeka Wakati Wa ujauzito Ili kumakomodeti Na Mtoto, Kuna wanaoendelea Kula namna Hy Kwa kuwa wamezoea Na kuendelea kunenepa, wengine wanapunguza sana Kula Ili wapungue. hayo ni maelezo yaliyopatikana Toka Kwa baadhi ya nnaowafaham.

ahsante mkuu!
 
Kunenepa ni kujiendekeza wadada, niwape tu mfano hai

Nilipojifungua nilikua na msichana wa kazi, wasichana wawili watoto wa dada zangu, mama yangu mzazi, (wasaidizi wangapi hao lol) basi nikajiachia mmama uvivu ukanijaa mtoto akilia najua kanyonya kashiba naita we mwafulani nachagua tu wako wengi njoo bembeleza mtoto huyu kashiba ananisumbua tu, na we fulani nilitee chupa ya uji, we mwingine nitafutie cd ile ya roze mhando na uniwekee wimbo no 3, ikiisha naita tena nibadilishie niwekee movie ya kinigeria mara niletee maji ya kuywa natuma mhindi kasingiziwa. Kilichonitokea usiombe kukutwa najuuuuuta mpaka leo.

Kupunguza mwili ni kazi kubwa sana labda uwe na matatizo yanakuandama itakusaidia ila ndio unaraha zako huli cha jirani utasota hasa. Eti unaambiwa kupunguza mwili usile kihepe,kitimoto unapita mahala kinakunukia hela unayo utaacha kula kweli! sidhani.

Uvivu uvivu uvivu wadada mijini unatuponza
 

hao wa vijijini wanamiili mizuri ila angalia sura zao wengi wanazeeka usoni! hawa wa mjini wengine ni kujitakia , wengine ni family planning, wengine ni kurithi, ila ukitaka kurud normal baada ya kujifungua unaweza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…