....Hunenepa sana baada ya kujifungua!

....Hunenepa sana baada ya kujifungua!

Chakula kinaongezeka Wakati Wa ujauzito Ili kumakomodeti Na Mtoto, Kuna wanaoendelea Kula namna Hy Kwa kuwa wamezoea Na kuendelea kunenepa, wengine wanapunguza sana Kula Ili wapungue. hayo ni maelezo yaliyopatikana Toka Kwa baadhi ya nnaowafaham.

ahsante mkuu!
 
Kunenepa ni kujiendekeza wadada, niwape tu mfano hai

Nilipojifungua nilikua na msichana wa kazi, wasichana wawili watoto wa dada zangu, mama yangu mzazi, (wasaidizi wangapi hao lol) basi nikajiachia mmama uvivu ukanijaa mtoto akilia najua kanyonya kashiba naita we mwafulani nachagua tu wako wengi njoo bembeleza mtoto huyu kashiba ananisumbua tu, na we fulani nilitee chupa ya uji, we mwingine nitafutie cd ile ya roze mhando na uniwekee wimbo no 3, ikiisha naita tena nibadilishie niwekee movie ya kinigeria mara niletee maji ya kuywa natuma mhindi kasingiziwa. Kilichonitokea usiombe kukutwa najuuuuuta mpaka leo.

Kupunguza mwili ni kazi kubwa sana labda uwe na matatizo yanakuandama itakusaidia ila ndio unaraha zako huli cha jirani utasota hasa. Eti unaambiwa kupunguza mwili usile kihepe,kitimoto unapita mahala kinakunukia hela unayo utaacha kula kweli! sidhani.

Uvivu uvivu uvivu wadada mijini unatuponza
 
Noted with thanks
mkuu!

Kaka nina dada yangu whom ni mkubwa kwangu kwa miaka almost mitatu whom
kutokana na kutokuchaguliwa kwenda shule za serikali enzi hizo na
familia yetu ikijishosheleza tu kwa mlo na kushindwa kumpeleka private
aliishia tu kuwa house girl wa wenye maisha bora town alipong'aria
shavu,thereinafter aliporudi kijijini akachukuliwa faster na then
shemeji yangu!

Frankly iliniuma kidogo wakati huo lakini muda unaponya majeraha,leo hii
dada yangu ana watoto wanne,ukiambiwa hata amezaa huwezi jua so far
kwenye family aliyoolewa ni yeye pekee ana jukumu la kutunza wakwe
zake,kutunza mji,kulea watoto,kutunza mifugo,kutunza shamba and likely!

Wenzake waliochaguliwa kwenda shule wakati wake waliishia form four/six
na kuunga hapa na pale kwa hutu tukozi nyemelezi,wamepata mabwana
wanaojua kuhudumia,wamezaa sana sana mtoto mmoja kisha kunenepeana
utadhani mbuzi wa hitma,kutembea kwenyewe taabu,wakipanda vitz inaenda
mwendo wa bata,kuhema juu juu utadhani uhai unataka kuwachomoka!

Yatosha kusema kwamba hawa wa kijijini kuna vitu wanakosa,exposure,umbea
wa saluni na haya mazaga zaga ya Mc Donalds ila wana span ndefu kuliko
hawa broilers! (samahani kwa vibonge) Huo ndio ukweli!

hao wa vijijini wanamiili mizuri ila angalia sura zao wengi wanazeeka usoni! hawa wa mjini wengine ni kujitakia , wengine ni family planning, wengine ni kurithi, ila ukitaka kurud normal baada ya kujifungua unaweza!
 
Back
Top Bottom