Takwimu Sahihi ni Kenya ana reserve ya 8.85 billion dollars naTanzania ana 5.18 billion dollars , Sasa kwamba wote tutakufa baada ya miezi mitano kama ndiyo akiba ya kuweza kuimport kwa nchi zote,Mimi siwezi kuongelea kitu hakijatokea tangu ulimwengu uumbwe( nchi iangamie kwa njaa kwa kukosa foreign reserve ) maana kuna mambo yatafanyika ili hill lisitokee. Hoja hapa ni yupi ana foreign reserve nyingi. Unaweza ukute nchi hata Italia aufano halisi Greece hana reserve ya miezi mitano lakini haiondoi ukweli kuwa wale ni kweli wamefilisika lakini hawajawa na maisha duni kama sisi Wa dunia ya tatu kwavigezo kama miundo mbinu yao, health care yao. Nk. Wewe unapoambiwa kuwa bajeti ya Kenya mwaka 2018 inazidi ya nchi tatu , Tanzania, Uganda, na Rwanda zote zikijumlishwa unaelewaje hiyo statement?. Hata Tanzania alikuwa tajiri kuliko Kenya hadi 1984 ndipo waliinuka kutuzidi hopefully huko mbeleni twaweza kuwazidi maana uchumi si kitu stagnant. Hamna anayefurahia kuzidiwa na Jirani kwa jambo lolote linalohusu maisha bora, lakini mwenzio akiwa mbele wewe ni kukiri tu halafu unaichukua kuwa ni changamoto ufanyeje ili umpite.