Nadhani kama Kenya wao wanajali mazao ya biashara zaidi,hii ni kuitazama kama fursa kwa Tz kuzalisha ‘mazao ya biashara’ ya kuiuzia Kenya yakiwa yameongezwa thamani tu.Badala ya kutupiana kejeli,nadhani bora na vema zaidi kuiangalia kama fursa ilimradi iwe na maslahi kwa Tz...'win win on both sides' kama ilivyozoewa kutamkwa.
Uchumi wa dunia ya leo ni wa kuangalia sana gharama.Kama kilimo cha hizo bidhaa huko Kenya ni ghali au ardhi haikidhi, vema kununua toka Tz(ama popote panapowafaa na wapaonapo ni rahisi).Si jambo baya.Cha msingi pesa ya kununulia iwepo tu.Hata makampuni makubwa ama hununua baadhi ya parts za tools/mashine zao toka nchi zingine (hata kama wangeweza kuzalisha wao,ila wakiona gharama itakuwa kubwa).Na hata pia huweza kuamua kufungua viwanda vyao kwenye nchi zingine,ilimradi kushusha gharama za uzalishaji na hatimae kuongeza faida yao.
Kama sikosei,ardhi yenye rutuba kwa Kenya, kwa kiasi kikubwa ilishawahiwa na walioiwahi,ambao nao hujizalishia wanavyoona vitawapa faida kubwa zaidi.
Kwenye shida ya nchi jirani yoyote,iwe imesababishwa na sababu yoyote ile,kama inafaa,ndio wakati mwafaka wa kuiangalia kama fursa,ambayo,si ajabu mbeleni ikazalisha na fursa zingine bora zaidi.