Huo ndio urithi wako wa pekee

Huo ndio urithi wako wa pekee

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kama una watoto, waombee, wakumbatie, wakikukosea wasamehe hata bila masharti; huo ndio urithi wako wa pekee!

Kuna watu wanatamani wangepata japo mtoto hata mmoja, lakini kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao hawajafanikiwa. Na wengine tayari ni wazee.

Watoto ni urithi wa pekee kutoka kwa Muumba wa mbingu na ardhi!
Wape thamani kuliko chochote ulichonacho!
Waambie unawapenda hata kama uliwapata pasipo kutarajia.

Usiwafanye kuchukia maisha waliyonayo. Wasaidie kujitambua,kujikubali na kujithamini hata kama wana kasoro.

Usikubali mtu yeyote aharibu urithi wako. Usiruhusu watoto wako kuitwa majina yasiyofaa.

Hata ikiwa kwa gharama zozote; linda urithi wako. Watoto wako, ndio urithi wako!

Wabarikiwe wote wanaowapa thamani watoto wao na kuwasamehe makosa yao pasipo masharti. Upendo wa dhati husitiri wingi wa makosa. Waombee heri watoto wako!
 
Usisahau kuwaadhibu wanapokosea wafundishe maisha kuna kupata na kukosa usiwadekeze wape kazi ngumu na nyepesi. Wafundishe kutunza pesa elimu ya dini kidogo isizidi kipimio, wafundishe technology na biashara, control taarifa anazozipata kwa njia ya television.
 
Wabarikiwe wote wanaowapa thamani watoto wao na kuwasamehe makosa yao pasipo masharti. Upendo wa dhati husitiri wingi wa makosa. Waombee heri watoto wako!
Amina..

Ila ni vyema kumuadhibu mtoto anapokosea kwa manufaa yake ya baadae.
 
Wakikosea niwasamehe hata bila masharti, una maana gani?

Watoto wafundishwe adabu, wakikosea wachapwe viboko na adhabu zingine zinazohimilika. Hili ni agizo la Mungu.

Unconditional love ni kitu chema, ila pamoja na huo urithi, usipoutumia urithi vizuri unageuka kuwa laana.
 
Umeandika Kama Mama, vizuri Sana.

Kama Baba hapo kwenye kuwaadhibu wanapokosea ni Jambo la muhimu zaidi kuliko yote.

Kwa maana usipowafundisha kuwaadhibu wanapokosea ili wakawa na tahadhari basi maisha yatawafundisha yenyewe kuwaadhibu na wataona dunia ni nzito
 
Usisahau kuwaadhibu wanapokosea wafundishe maisha kuna kupata na kukosa usiwadekeze wape kazi ngumu na nyepesi. Wafundishe kutunza pesa elimu ya dini kidogo isizidi kipimio, wafundishe technology na biashara, control taarifa anazozipata kwa njia ya television.
Hii comment ndio inayobeba thread nzima na bila haya uliyoyaeleza huo upendo hautazaa matunda mema,kila mzazi anawapenda watoto wake lakini yaliyobeba comment hii yakizingatiwa yataleta matunda mema kadhalika upendo bila control ni hatari sana,sometimes inabidi mzazi u act ukauzu kidogo hasa pale watoto wanapofanya ndivyo sivyo
 
Watoto sio Urithi
Urithi ni mali, pesa, ardhi
 
Wakikosea niwasamehe hata bila masharti, una maana gani?

Watoto wafundishwe adabu, wakikosea wachapwe viboko na adhabu zingine zinazohimilika. Hili ni agizo la Mungu.

Unconditional love ni kitu chema, ila pamoja na huo urithi, usipoutumia urithi vizuri unageuka kuwa laana.
Masharti ni kama vile kumfukuza binti baada ya kupata ujauzito au kijana anapokataa shule na kuwaacha wanatanga tanga mtaani kama asiye na wazazi.

Au kumtamkia maneno ya kukatisha tamaa na kuvunja moyo. Mfano mtoto ameharibu kitu fulani, kuna baadhi ya wazazi huwaambia maneno magumu sana watoto wao.
"Hilo gari sio lako ni langu"
"Usiniharibie nyumba yangu wewe ni mpitaji tu" nk
Maneno kama hayo huweza kumtenga mtoto mbali na mzazi hasa anapopata uwezo wa kujitegemea.

Ndio maana leo hii kuna baadhi ya watoto hawaendi kwa wazazi wao mara kwa mara na wakienda hukaa siku chache. Ukifuatilia utagundua ni matokeo ya malezi wakati wa utoto!
 
Back
Top Bottom