Huruma, Mathare imegeuka uwanja wa maandamano kwa siku ya tatu baada ya wakazi kuandamana wakitaka vijana wawili waliopotea, Abdulaziz Duba Molu almaarufu Zizo na Maxwell Kiarie, wapatikane.
Maandamano hayo yaligeuka kuwa machafuko baada ya polisi kukabiliana na waandamanaji kwa kutumia teargas huku mtu mmoja akipigwa risasi na kufariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa.
Barabara kadhaa ikiwemo Outer Ring Road zilifungwa kwa mawe na vizuizi kwa saa kadhaa, hali iliyosababisha biashara kufungwa na usafiri kutatizika. Wakazi pia walidai baadhi ya watu waliibiwa wakati wa vurugu hizo.
Police walisema baadhi ya waliojeruhiwa walikuwa wakihusika na uporaji na kushambulia wananchi pamoja na kuziba barabara. Hata hivyo, afisa mwingine wa polisi alisema uchunguzi unaendelea kubaini mazingira ya tukio la ufyatuaji risasi.
Kisa kikubwa kinachozua hasira ni kutoweka kwa Zizo na Maxwell, ambao familia na marafiki wanasema walichukuliwa wiki iliyopita lakini hadi sasa hawajafikishwa mahakamani wala hakuna taarifa rasmi kuhusu walipo.
Wakazi wanashuku kuwa huenda wanashikiliwa na maafisa wa serikali, madai ambayo hayajathibitishwa rasmi.
Zizo si jina geni kwa polisi. Mwaka 2024 aliwahi kukamatwa katika operesheni iliyovunja genge lililodaiwa kuhusika na wizi wa bunduki kutoka kwa wamiliki halali. Polisi walidai uchunguzi ulihusisha wanawake waliokuwa wakiwalewesha waathiriwa katika vilabu kabla ya kuwaibia bunduki na mali nyingine.
Katika operesheni hiyo, bastola mbili na risasi zilipatikana, huku moja ya bastola hizo ikidaiwa kuwa ilikuwa imeibwa kutoka kwa afisa wa polisi.
Licha ya historia hiyo, familia na marafiki wa Zizo wanasisitiza kuwa ikiwa alikamatwa, anapaswa kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria badala ya kutoweka bila maelezo. Maandamano yanaendelea huku wakazi wakitaka ukweli ujulikane kuhusu alipo Zizo na Maxwell.
Source : TheStar.co.ke