"Huruma yako inaweza kuwakaribisha na kuwalea maadui"

"Huruma yako inaweza kuwakaribisha na kuwalea maadui"

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara (53)✍️
Binadamu anapaswa kuwa na huruma kwa binadamu mwenzake, lakini ahakikishe huruma yake ina kiasi. Usiwe na huruma kupita kiasi kwani unaweza kuwakaribisha na kuwalea adui hatarishi.

Adui wengine hupita kwenye mlango wa huruma, kila mara atahitaji msaada wako hata kwenye jambo ambalo lipo chini ya uwezo wake ili aweze kukukaribia zaidi na kufahamu mengi kuhusu wewe. Kwasababu ya huruma yako adui atajenga ngome yake kwenye himaya yako. Hakika atakuwa anakushambulia pasipo kumjua ni nani anayekushambulia.

Bila shaka adui atakuadhibu vibaya mno kupitia huruma yako huku ukidhani yeye ni rafiki mwema, yawezekana hutoacha kuomba ushauri kwake kuhusu magumu unayopitia.

Right Marker
Dar es salaam
 
Back
Top Bottom