Kwa level yako sikutegemea uchangie ivi, kuna watu wanaongoza kutapeli kama Hao whites uko? Mana wewe sijui ukisema crime sijui unamaanisha nini mana hata mikataba tu ya nchi zetu na ukoloni vyote ivo ni crime, Ngombe wanazaliwa kila siku
Mkuu, nakuomba chondechonde usiniweke level yoyote, kwa sababu ukiniweka level fulani unaninyima uhuru wangu wa kuwa level yotote.
Mimi nathamini zaidi uhuru wangu wa kujieleza ninavyoona kuliko kuwekwa level fulani na wewe.
Huyu Hushpuppi kafulia.
Kafulia kwa watu wanaohalalisha upigaji, kafulia kwa watu tusiohalalisha upigaji.
Kwanza kabisa, kumtetea kwa " hao whites wanaongoza utapeli" kama unavyosema wewe, ni kukosa uwezo wa kuchambua na kuifanya hii ni ussue ya identity politics. Hawa WaNigeria si some modern day Robin Hood wanaowaibia wazungu tu, hata kama hilo lingekuwa ni right. Hawatapeli whites tu, wanapiga hata kwao, zaidi two wrongs do not make a right.
So, lets get that right.
Zaidi, hata kama ukisema unahalalisha upigaji wewe mvaluvalu hujali dini wala utamaduni wala siasa, unajali kupiga hela tu, sawa.
Lakini, kwa mtu yeyote asiyejua au kuweza kufanya "self preservation" akapiga hela kubwa, akashindwa kujizuia kuwa "under the radar" na "off the grid", akakamatwa, huyo kafulia.
Kwa sababu, kaweza kazi ngumu ya kupiga hela kubwa, halafu kashindwa kazi rahisi ya kuzuia nyege zake za kujionesha machoni pa watu kwamba yeye kapiga hela kubwa.
Hii Kiswahili tunaita "ujanja mwingi, mbele kiza".
Hapo nimemaliza kwa mabaharia valuvalu wasiojali la muazini wala mchota maji msikitini, wao wanajali kupiga pesa tu.
Kwetu sisi tunaojali maadili, tunaoangalia pesa zimepatikanaje, sio kujali pesa tu, tunaojali miiko ya maana ya kijamii, tusiotaka kuiba, tusiotaka kuishi kwa hofu, tunaotaka tuwe na uwezo wa kutamba na mali zetu bila hofu ya kushikwa (hata kama hatufanyi hivyo kwa sababu nyingine za kimaadili na kiusalama), mtu kujiingiza katika maisha ya wizi na utapeli ni kukubali kushindwa maisha. Bila kujali kwamba mtu huyo anakamatwa au hakamatwi.
Mimi naamini kwamba, kama una uwezo wa kutapeli watu dola za kimarekani Milioni 40, kwa akili hiyo hiyo uliyotumia kutapeli nje ya sheria, ukijipanga vizuri, unaweza kutengeneza dola za Kimarekani milioni 400, kisheria, hata kama ni kwa kuwapiga watu kisheria tu.
Kwa hiyo Hushpuppi kafulia kwa sababu kakamatwa, kwa wasiojali maadili wanaojali hela tu.
Kwetu sisi wengine, tunaojali maadili, hata kama asingekamatwa, tungeweza kusema "hizo hela hata matajiri wa Forbes hazihesabiwi, kwa sababu zinajulikana ni hela chafu, hazina heshima".
Vyovyote utakavyoamua kumuangalia Hushpuppi, kishua ama kisela, amefulia.
Suluhu yake sasa hivi ashinde kesi, kitu ambacho Mmarekani hawezi kuruhusu na hata kama ikitokea, reputation yake ishaharibika vibaya sana.