BASHE AENDELEA KUHAMASISHA TAASISI ZA FEDHA KUTOA MIKOPO YA RIBA NA MASHARTI NAFUU KWA WAKULIMA; UJENZI WA MAGHALA NA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI BAADA YA KUKUTANA NA MENEJIMENTI YA BENKI YA EQUITY
Dodoma, Tanzania.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amekutana na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Benki ya Equity nchini, ambapo katika mazungumzo hayo ameishauri menejimenti hiyo kuongeza mitaji katika Sekta ya Kilimo hususani katika uwekezaji kwenye ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji na Maghala.
Mazungumzo hayo ambayo yamefanyika katika Ofisi ya Waziri, Jijini Dodoma huku Ujumbe wa Benki ya Equity ukiongozwa na Bi. Isabela Maganga ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo hapa nchini.
Aidha Bi. Isabela kwa niaba ya benki hiyo amemuahidi Waziri Bashe kuwa wapo tayari kutoa ushirikiano na kusaidia Serikali katika kukuza Sekta ya Kilimo nchini.
Mkurugenzi huyo pia aliongozana na; Raphael Onyango (Mkurugenzi wa wateja wakubwa-makao makuu Kenya) pamoja na Aboubacar Youssoufou- Mkurugenzi wa Mikopo -Makao makuu Kenya).
#Ajenda10/30
#KilimoBiashara