Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 15 leo Aprili 28, 2023.
Serikali imesema haiwezi kudhibiti bei ya mazao, bali inapunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima pamoja na kuongeza tija kwenye uzalishaji ili wakulima waweze kupata faida baada ya gharama zao kupungua.
Haya yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akijibu swali la Esther Edwin Maleko, Mbunge wa Viti Maalum aliyetaka kufahamu namna ni kwa gani Serikali inafanya ili kudhibiti bei ya Kahawa ambayo imekuwa inapanda na kushuka kila siku.
Aidha, Serikali inapanga kuhamasisha matumizi ya kahawa ndani ya Nchi pamoja na kuongeza uwekezaji kwa baadhi ya viwanda, mfano maeneo ya Kagera ambapo uwekezaji kwenye Kiwanda cha TANICA utaongezwa ili kuongeza ubora na kutoa uhakika wa bei nzuri kwa wakulima.
Pia, Waziri Bashe amesisitiza kuwa kuanzia mwaka 2025/26, Tanzania itaacha rasmi kusafirisha nje ya nchi korosho zisizo banguliwa kwa kuwa zote zitabanguliwa kwanza nchini.
GAMBO AKOSOA MFUMO WA UTOAJI LESENI BIASHARA YA VITO
Mbunge Mrisho Gambo amesema “Kuhusu wafanyabishara wa vito, watengenezaji na wauzaji wa bidhaa za sonara Nchini, ukiangalia Sera ya Madini ya Mwaka 2009 inasisitiza Wananchi wote kuongeza thamani ya madini lakini inapishana na matakwa ya Kisheria.”
Amesema ili mtu aweze kufanya biashara ya sonara anatakiwa kuwa na leseni tano, hali ambayo anaona haipo sawa na kudai kuwa ukijumlisha gharama zote za kukata leseni inakuwa ni zaidi ya Tsh. Milioni 13.