GE2025 Hussein Bashe: Tutauza sukari nje kwa sababu ni biashara na sio huduma

GE2025 Hussein Bashe: Tutauza sukari nje kwa sababu ni biashara na sio huduma

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mgombea wa Ubunge wa Nzega Mjini ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake haiwezi kukataa kuuza sukari nje ya Nchi Kwa sababu kuna baadhi ya watu wanaohoji kwanini Tanzania inauza sukari Nje ya Nchi kwamba Kutakuwa na upungufu wa Bidhaa hiyo

Bashe ameyasema hayo leo Oktoba 16,2025 katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba Mkoani Kagera kwenye mwendelezo wa Mikutano ya Kampeni za uchaguzi Mkuu 2025 ya Mgombea wa kiti Cha Urais Kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan

Bashe amesema kuwa hizo ni Lugha za kisiasa kwamba Kutakuwa na upungufu wa Sukari,Sekta ya Kilimo Dkt. Samia ameshatoa sera na suala Hilo ni biashara na wala sio Huduma hivyo kama Kuna Nchi zitahitaji Sukari watawauzia.
 
Whole system is rigged for the rich, we just the ones paying the price
 
Faida ya hayo mauzo yanatusaidia vipi ? Unless watawaongezea wakulima malipo ya mauzo ya Miwa. Sioni haya mambo ya msaada gani...; Hawa jamaa bila Matozo yao mambo yangekuwa bora zaidi....

 
Back
Top Bottom