Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo: Waagizaji hawakupaswa kuleta mchele wa Msaada kutoka Marekani kwani Tanzania ina hazina ya mchele

Unasema mchele upimwe? Kama hao jamaa wameweza kuuleta hadi umefika Bongo, unadhani kuna uwezekano wa kuukagua? Nani athubutu?

Kwa lugha rahisi tu ni kwamba Mmarekani anafanya anachotaka yeye; sie tutabaki wapiga-kelele tu.

Kifupi, viongozi wameshatuuza tayari.
 
Tena angekuwa uncle Magu viongozi wa hiyo NGO wangekula mboko, wanataka kutuulia kizazi chetu shupavu. Hii nchi ina watu wa hovyo sana, ilitakiwa wapewe masaa kadhaa huo mchele uwe umechomwa na TBS
Usihadaike na maneno ya huyo Msomali. Hii nimkshifa kubwa na inamhusu, uungwana ni Kujiuzulu tu tena haraka mno
 
Umesema vyema. Kuna watu akili zao ziko tenge tangu kuzaliwa.

Wameona Tanzania ndio nchi inayoweza kupokea misaada bila kuhoji.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alikuwa wapi vyakula hivi vikigawanywa huko Dodoma hadi lilivyoibuliwa Jf?
 
Serikali ijiridhishe? Mpaka imeruhusu mchele umeingia nchini, unadhani nini kitabadilika?

Nani mtaalamu atakayekuwa tayari kulitia dosari taifa la Marekani, iwapo kuna uwalakini kwenye huo mchele?
 
Ulipitia wapi hadi umefika Dodoma? Kwani Tanzania inaruhusu kuingiza Mchele? Changa la macho baada ya kuona reactions za watanzania.
 
Swali jee utafiti umefanywa kuhakikisha hivyo virutubisho ni vizuri kwa watoto wetu, visine kuwa na Virutubisho vya kujenga marekebisho ya JINSIA ya Vijana kuwa vinginevyo. Maana siku hizi kuna hila za kupunguza idadi ya watu, haswa barani Africa
Au inawezekana ni virutubisho vya majaribio.

Watanzania wanageuzwa kuwa Guinea Pigs!
 
Hata vifaru na zana za kijeshi vinapitisha nchini .

Jana nimekutana na msafara wa magari ya Uganda ukitokea bandari ya Tanga, kupitia huko Arusha na Kilimanjaro kuelekea Uganda.

Mizigo iliyokuwa imebebwa ni mungu anajua, tena escort ya police wa TANZANIA ilikuwa mbele kulinda na kusindikiza huu mzigo.
 
kwahiyoBashe hadi unaagizwa na NGO yeye alikuwa hajui kweli?
Alikuwa anajua, ila sema tu hana meno ya kung'ata. Ndiyo maana analilia tu kama sie.

Hayo ndiyo madhara ya kutegemea mikopo na misaada ili kuendesha nchi.

Hapo lazima wafadhili wajiamulie wenyewe nini wafanye.
 
Mbali ya hicho chakula, mbona kuna miradi lukuki inayofadhiliwa na USA na hatujaona serikali ikijishaua hivyo. Bashe aache uswahili, tatizo si uwepo wa mchele, tatizo ni uwezo wa kaya (purchasing power) nyingi kuafford huo mchele, na hii ni dalili ya jamii iliyojaa ufukara..
 
Kwani imewahi kutokea mzungu akampenda mtu mweusi??? Tukienda huko kwao wanatuita nyani na kutunyanyapaa kila kona. BTW mzungu anatafuta kila namna kumpoteza mtu mweusi kwenye uso wa dunia.

Tunalindwa na Mungu tu
 
Tena angekuwa uncle Magu viongozi wa hiyo NGO wangekula mboko, wanataka kutuulia kizazi chetu shupavu. Hii nchi ina watu wa hovyo sana, ilitakiwa wapewe masaa kadhaa huo mchele uwe umechomwa na TBS
Tungekuwa na rais mwenye akili huo mchele usingeingia kabisa. Bashe na mamake hamnazo kabisa
 
Lakin pamoja na Yote maabara zetu zinashindwa kbsa kupma huo mchele una nn ndan , Watu wanapng tuu utazan n story za vijiwen
 
Sehemu chakula kinapotoka lishe ni duni. Shida ni elimu sio uhaba
Elimu juu ya lishe sahihi inaweza kuwa sehemu ya tatizo, lakini yapo matatizo lukuki mbali ya hiyo elimu. Mojawapo ni uwezo wa kumudu hicho chakula kwa mwaka mzima, sana sana wakati wa mavuno inawezekana ila baada ya hapo ni maisha ya kubangaiza.
Matatizo ya kijamii inaweza pia kuwa tatizo jingine, wakati wa mavuno anayekwenda kuuza mazao ni baba wa familia, akishauza matumizi yanakuwa si mazuri, baada ya muda hakuna pesa ndani, wanaotaabika ni mama na watoto kwa kuanza kuokoteza vyakula mashambani.
Kwa umasikini huu si rahisi kaya nyingi zikapata lishe bora kwa msimu mzima, hata ukizipa elimu ya kutosha mabadiliko yatakuwa kidogo hasa kwa zile kaya zenye kujiweza kwa msimu mzima.
 
Kwani imewahi kutokea mzungu akampenda mtu mweusi??? Tukienda huko kwao wanatuita nyani na kutunyanyapaa kila kona. BTW mzungu anatafuta kila namna kumpoteza mtu mweusi kwenye uso wa dunia.

Tunalindwa na Mungu tu
Marekani sio wazungu tu.
Wako watu wa kila jamii na rangi, Waziri wa Ulinzi na Balozi wa US hapa nchini ni weusi kuliko wewe.
 
Sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…