Hussein Mwinyi kuitwa Rais Mteule kabla hajachaguliwa na wananchi ina maana gani?

Ndio maana watu wanataka tume huru ya uchaguzi ,hata hayati Rais mstaafu Mkapa alisema.
 
Wacha wampe kila wanachoweza kumpa, lakini urais Zanzibar mwaka huu ni wa Maalim. Hakuma mwenye uwezo wa kuzuia hilo.
 
Hebu leta hiyo clip akiitwa rais mteule
 
Utabisha tu lakini Mwinyi ndiye Rais wa Zanzibar. Hicho kibabu cha kujirudia kila uchaguzi, wapiga kura wamekichoka.
Habishi ila anauliza kuitwa Rais Mteule kabla ya Uchaguzi imekaaje?
 
Tuliza tako dawa ikuingie vizuri, Mwinyi ndie Rais wa Znz, bwana Sawa Sawa anamsindikiza tu.
Acha matusi ni utoto huo halafu kama huna hoja kaa kimya sio lazima kucomment Matusi yanakuonyesha tabia yako.
 
Ndio Ni Raisi mteuliwa kateuliwa na wajumbe wa CCM mkutano mkuu wa CCM
Angeapishwa basi hebu tumia akili kidogo tu ccm ilimteua kama mgombea wao sio Rais mteule hili nalo haliitaji uwe na degree kama Mzee wetu Mwakyembe hata ukiwa Mjumbe tu utalijua
 
Kazi ya CCM ni kuteua Rais

Kazi ya Tume ni kuandaa na kusimamia mchakato wa wananchi kubariki maamuzi ya Chama
 
Utabisha tu lakini Mwinyi ndiye Rais wa Zanzibar. Hicho kibabu cha kujirudia kila uchaguzi, wapiga kura wamekichoka.
Mwendelezo wa mambo ya kienyeji ya ccm na serikali yake.
 
Akina Jecha ndiyo watangaza matokeo hapo unategemea nini. Huoni keshapewa body guard tayari .... Hiyo ndiyo CCM!!
 
Rais wa Zanzibar alishachaguliwa na wana-CCM wa Tanganyika kule Dodoma, kilichobakia ni kutimiza matakwa ya kisheria tu ili aapishwe na kuhamia Ikulu ya Zanzibar
 
Ina maana kuna watu ni washamba kama mh Zitto alivyosema.
 
Kuna kijamaa kimoja kwa sasa kimekuwa bonge kipo kati ya walinzi wa Magufuli, kilianza kumlinda magu tangu alipoteuliwa na ccm kuwa mgombea 2015.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…