Leonardmwanja
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 236
- 35
Walioiba wamepata aibu ya mwaka kumuibia hata kijana wao.Hakuna kuangalia uso pengine wangejua ni mzawa wa pale.Wao mtaji wao ajali aibu kubwa watajaimbia baba zao
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu,
Wow, mbona umenishitua unaposema jambo la kawaida kabisa. Yaani kwa Tanzania marehemu kuibiwa mpaka nguo alizovaa?
Mawazo ya kusema "Watu maarufu wakiibiwa vitu vyao kwenye ajali ndiyo Serikali itoe tamko" hilo sikubaliani nalo, hapa tunajenga na kukemea maovu kama hayo,Mkuu wa Wilaya katoa tamko sahihi. Waliofanya ujinga huo kwa kumuibia maiti, Mwenyezi Mungu awape pigo takatifu hapa hapa Duniani. Insha allah.
Hayo mambo ni ya kawaida kwa wanavijiji wanaoishi pembezoni mwa barabara kuu zote sirikali inalitambua hilo! Nchi inaangamia.
SERIKALI wilayani Muheza imetoa muda wa saa 24 vinginevyo italazimika kutumia nguvu ya dola kuwasaka na kuwafikisha mahakamani wananchi wote wa Kijiji cha Songa Kibao Maguzoni waliohusika na wizi
wa mali za Msanii Hussein Ramadhan Mkieti 'Sharo Milionea', aliyezikwa jana Lusanga Muheza.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Muheza ,Subira Mgalu, wakati akitoa tamko la Serikali kutokana na aibu hiyo iliyojitokeza wakati wa tukio la ajali ambapo msanii huyo aliibiwa mali zote ikiwa ni pamoja na nguo alizovaa.
Alisema Serikali itatumia nguvu kuwasaka watu hao kwa sababu inajulikana waliohusika na wizi huo na kutahadharisha kuwa wajisalimishe wenyewe kabla hatua ya kuvamia kijiji hicho
na kutumia nguvu ya dola haijafanyika.
Mgalu alitoa saa 24 kuhakikisha vitu vyote vilivyoibwa vinasalimishwa na baada ya hapo nguvu itatumika kuwasaka
watu wote na watakamatwa na kufikishwa Mahakamani.
Mwandishi,
Benedict Kaguo
Kutoka gazeti la Majira
ANGALIZO:
Watanzania kama tumefikia kiwango hiki cha kutokuwa na hekima na huruma basi tunakuwa kama taifa mfu. Umaskini siyo sababu ambayo inatufanya tufikie kiwango hiki cha fikra na matendo yasiyo ya kibinadamu mwenye akili timamu.