Hussein Ramadhan'Sharo Milionea' aibiwa nguo zote alizokuwa amevaa kabla ya ajali.

Walioiba wamepata aibu ya mwaka kumuibia hata kijana wao.Hakuna kuangalia uso pengine wangejua ni mzawa wa pale.Wao mtaji wao ajali aibu kubwa watajaimbia baba zao
 
Mkuu Ng'wamapalala unashangaa !,huku Arusha ukiharibikiwa gari usiku maeneo ya kwa mrefu,Shangarai,chama,kwapoli....utajuta na utakubali kweli kuna waTanzania wengi wanaishi chini ya dola moja kwa siku.

Mkuu,
Wow, mbona umenishitua unaposema jambo la kawaida kabisa. Yaani kwa Tanzania marehemu kuibiwa mpaka nguo alizovaa?
 
Last edited by a moderator:
hata kama tukisema ni hali ya kawaida lakini haina sifa nzuri jaribu kupata picha kwa mfano nguo za marehemu (Sharobaro) alizokuwa *amevaa ile picha iliyokuwa haina maadili inaonyesha mwili ulikuwa umejaa damu na zile ni nguo zilizokuwa nje je zenyewe hazikuwa na damu? na kama zilikuwa na damu anaenda kuzitumia vipi aliezipata? inasikitisha eti jamaa kapiga simu halafu kamaliza anasema wape taarifa na wengine sababu hii simu ni yangu sasa na haitaonekana tena
 
Mawazo ya kusema "Watu maarufu wakiibiwa vitu vyao kwenye ajali ndiyo Serikali itoe tamko" hilo sikubaliani nalo, hapa tunajenga na kukemea maovu kama hayo,Mkuu wa Wilaya katoa tamko sahihi. Waliofanya ujinga huo kwa kumuibia maiti, Mwenyezi Mungu awape pigo takatifu hapa hapa Duniani. Insha allah.
 

It's so sad.

Kuna wengine humu eti wanaona hili tamko kama vile serikali inajaribu kuzika habari na mijadara muhimu kwa kushupalia issue hii.

Hii inaonyesha ni jinsi gani watu wanaadhilika kifikra kwa kulishwa fikra mbaya za kisiasa ambapo kwa sasa kila jambo kwao ni siasa.

Jamii ya Kitanzania inakuwa kama taifa mfu. Watu hata huruma kwa sasa hawana achilia mbali huzuni.
 
kwa kuwajuza tu,matukio ya kuibiwa wakati ukipata ajali ni vitu tulivyovizoea kwa miaka mingi sasa,na kwa ushauri tu ukipigwa search baada ya ajali bora ujifanye umekufa mambo yaende kiusalama ukikohoa tu wezi wanakumalizia!!!
(tatizo hili imefika wakati litafutiwe ufumbuzi wa kina)
 
Tanzania kama Taifa tunatia aibu sana. tumekuwa wanyama. Hili ni tatizo ambalo ni rahisi kabisa kulikomesha lakini Polisi wanafanya kama vile halipo. Mimi nadhani hili tatizo serikali itaamua kulizima pale tu atakayepata ajali awe mtu mzito serikalini kama waziri halafu aibiwe au auawe ili aibiwe. Kama taifa tunatisha kwelikweli. Kuna wale akina mama wa Kenya walipata ajali karibu na Wami walifanyiwa unyama wa kutisha.

Mimi na mke wangu tulipata ajali Zambia kwenye kijiji kimoja kinaitwa Mlilima. Gari yetu ilipasuka gurudumu na kuviringika mara tatu huku likitupa vitu vyote vilivyokuwa ndania ya gari. Mungu alitusaidia hatukuumia. Wanakijiji walikuja kwa wingi sana kwenye eneo la ajali na walikusanya vitu vyote vilivyokuwa vimezagaa sehemu ya ajali na kutupatia. Tanzania tungeuawa siyo na ajali bali na watu ambao wangetaka kutuibia hadi nguo zetu.

 
Mwaka 2010 mwezi wa 10 nikiwa natoka Tabora nilipata ajali katikati ya Morogoro na Dodoma, Ilikuwa muda wa saa 10.45alfajiri,nilichoshangaa ndani ya dk 10 watu walikuwa wameshajaa eneo la tukio, watu wa eneo lile ni watu wapekee sana kwani walinisaidia sana pamoja na wenzangu nilioongozana nao!! Polisi wa Dumila walifanya kazi nzuri sana! Na Mimi siyo mtu maarufu,ingawa palitokea watu wachache waliotamani kudokoa vitu vyetu lakini wananchi walikuwa makini sana!! Natamani watu wa Muheza wangekuwa Kama watu Wa kijiji cha Magubike!!RIP Sharo!!
 
Mkuu wa Wilaya alitakiwa asitoe tamlko lolote kuhusu kuibiwa marehemu. Sana sana alitakiwa amkumbushe Kamanda wa Polisi afanye kazi anayotaklwa kufanya - kimya kimya na mahakama zifanye kazi yake. Tamko lingetolewa baada ya kuwanasa waliofanya huo unyama na kile amabcho wamefanyiwa hao wahalifu ili liwe fundisho.
 
Hata watu wa mjini wanafanya haya mambo!

Hayo mambo ni ya kawaida kwa wanavijiji wanaoishi pembezoni mwa barabara kuu zote sirikali inalitambua hilo! Nchi inaangamia.
 
Miaka 6 baadae, endelea kupumzika kwa amani kaka
 
siku zinakwenda aiseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…