Hutakiwi kuwa na hofu ya Mungu unatakiwa kumuheshimu, kumcha na kumpenda

Hutakiwi kuwa na hofu ya Mungu unatakiwa kumuheshimu, kumcha na kumpenda

secretarybird

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
2,998
Reaction score
4,948
Naomba hii dhana ya hofu ya mungu ifutike mara moja na isijirudie tena, mungu hutakiwi kumwogopa bali unatakiwa kumuheshimu na kumpenda kwa maana mungu siyo mbaya na Hana nia mbaya kwetu.

Nimeshakutana na watu wanasema natafuta mwanamke mwenye hofu ya mungu pia kuna baadhi ya wazazi wanawatishia watoto wao kuwa Mungu atawachoma endapo watafanya makosa fulani.

Juzi nilicheka na nikasikitika kwa wakati mmoja baada ya kusikia mzazi mmoja akimwambia mtoto wake "kunywa uji usipokunywa mungu atakutupa kwenye tanuru la moto".

Nambeni sana msiwafanye watoto wenu wamwone mungu ni mbaya na adui.

Hayo niliyoende kujifunza baada ya Mods kunipeleka kwenye fungate ya takriban siku mbili kwa hisani ya Minjingu Jingu.
 
Una ushahidi wowotwa kwamba Mungu hatoenda kuwachoma waliomkosea? Na nadhani hofu ya Mungu unaitafsiri tofauti.
 
Una ushahifi wowotwa kwamba Mungu hatoenda kuwachoma waliomkosea ?na nadhani hofu ya Mungu unaitafsiri tofauti .
Hata kama anaenda kuwachoma tisiwatishie watoto mpaka wakahisi mungu ni mbaya bali tuwahashe kumpenda.

Mtoto mdogo akiamini kuwa Mungu anawachoma watu Moto wanaongeza hofu ndipo nidhamu ya woga inatawala.
 
Mambo ya imani yako overrated
Mwenyezi MUNGU twatakiwa kumpenda, kumcha, kumweshimu, kumshukuru, na kumuomba yeye ni BABA, muumbaji wetu, mwokozi, mmiliki wa nchi na vyote viijazavyo.

Tunatakiwa kumpenda na sio kumwogopa upendo wa hofu sio upendo ufaao
 
Mambo ya imani yako overrated
Mwenyezi MUNGU twatakiwa kumpenda,kumcha,kumweshimu,kumshukuru, na kumuomba yeye ni BABA,muumbaji wetu,mwokozi,mmiliki wa nchi na vyote viijazavyo
Tunatakiwa kumpenda na sio kumwogopa upendo wa hofu sio upendo ufaao
Mukuu makanisa ya leo yanaaminisha watu mungu anakiwa kuogopwa
 
Back
Top Bottom