HUU HAPA MGOGORO WA SONGORO MARINE NA WAHANDISI

HUU HAPA MGOGORO WA SONGORO MARINE NA WAHANDISI

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
165
Reaction score
181
UTAPELI UNAOFANYWA NA KAMPUNI YA SONGORO MARINE WAWEKWA HADHARANI

Kampuni ya Songoro Marine ya Ilemela jijini Mwanza inakabiliwa na tuhuma za kujipatia zabuni tatu za kujenga meli katika maeneo mbalimbali hapa nchini bila kuwa na sifa zinazohitajika kitendo ambacho kinatajwa ni cha uhujumu uchumi.

Kampuni hiyo inayomilikiwa na Major Songoro ni miongoni mwa kampuni za kizawa zinazopewa zabuni na serikali mara kwa mara kujenga vivuko maeneo mengi hapa nchini ila kwa sasa imebainika ni miongoni mwa kampuni zinazofanya kazi kwa njia ya udanganyifu.

Kampuni ya Songoro marine imekuwa ikitumia majina ya wahandisi hewa ambao wengine walishaacha kazi kwenye kampuni hiyo lakini bado inaendelea kutumia vyeti na majina yao kuomba kazi serikalini ikifahamu ni kosa kisheria.

Katika nyakati tofauti kampuni hiyo ikiwemo mwaka 2023/2024 ilijipatia kazi ya kujenga meli ya MV Panga 11 mkoani Tanga yenye zabuni namba ( Tender No. X8/2023/2024/W/55) katika zabuni hiyo kampuni hiyo ilishinda.

Kampuni hiyo pia mwaka huo huo ilipata kazi ya kujenga kivuko cha Kigamboni ( Tender No.X8/2023/2024/W/53)

Kazi ya tatu ni ya mwaka 2023 na 2024 ya ujenzi wa MV. Mafanikio ( Tender No. X8/2023/2024/W/54.

Inaelezwa Songoro marine ilijipatia kazi hizo tatu za maeneo mbalimbali nchini kwa njia ya udanganyifu kutokana na kuwasilisha jina la Mhandisi William Deogratius Basiga bila kuwa na makubaliano nay eye wala kampuni ya Basiga.

Imebainika kampuni ya Songoro ilitengeneza barua pepe feki inayonesha ni ya mhandisi Basiga ili taarifa zote zinazotumwa ziweze kupita kwenye kampuni hiyo jambo ambalo ni la uongo.

Mhandisi Basiga ambaye jina lake liliwasilishwa PPRA na kampuni ya Songoro marine ikionekana ni mtumishi wa kampuni hiyo ili kupata zabuni za ujenzi wa meli hizo tatu lakini ukweli ni kwamba Mhandisi Basiga ni mmiliki wa kampuni ya AQUARIAN Project Solution.

Taarifa zilizopo zinaeleza kuwa kutokana na udanganyifu huo wa Songoro Marine kutumia jina lake na kujipatia zabuni za mabilioni ya fedha, tayari Mhandisi Basiga ameiandikia Songoro Marine barua ya kuomba fidia.

Kutokana na kampuni ya Songoro kutumia jina la Mhandisi Basiga bila makubaliano, Basiga kupitia wakili wake waliandika barua Septemba 7, 2024 kudai fidia kiasi cha shilingi 3,500,000,000 pamoja na asilimia tano ya miradi yote mitatu.

Baada ya barua hiyo, kampuni ya Songoro ilijibu barua Septemba 13, 2024 na kukiri kufanya makosa hayo na kueleza kuwa hawatafanya makosa mengine na kuitupia lawama Temesa.

Inadaiwa kuwa mkurugenzi wa Songoro marine kupitia wakili wake licha ya kukiri kufanya makosa hayo walionyesha kutoa vitisho dhidi ya mhandisi Basiga wakimtaka asiendelee kufuatilia jambo hilo.

Hata hivyo, taarifa za kughushi nyaraka hizo na kujipatia zabuni, zimefika Mamlaka ya ununuzi wa Umma PPRA ambao walikiri kampuni ya Songoro Marine kutumia jina la mhandisi Basiga kuomba zabuni hizo tatu.

PPRA iliahidi kuchukua hatua za haraka kwa kampuni ya Songoro marine kwa kutumia wahandisi ambao sio waajiriwa lakini tangu kipindi hicho mpaka sasa hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa.
 

Attachments

  • IMG_0365.jpeg
    IMG_0365.jpeg
    442.6 KB · Views: 1
  • IMG_0366.jpeg
    IMG_0366.jpeg
    659.8 KB · Views: 1
  • IMG_0367.jpeg
    IMG_0367.jpeg
    651.8 KB · Views: 1
  • IMG_0368.jpeg
    IMG_0368.jpeg
    452.7 KB · Views: 1
Je, ukiondoa hilo suala la wahandisi! Vivuko na Meli zote walizotengeneza zina shida gani mpaka sasa?

Maana isije ikawa hawajotoa 10% na hivyo mkaona muwasagie kunguni. Wabongo wengi uzalendo 0! Mko radhi muwape wageni hizo zabuni za kujenga vivuko, kuliko kuwapa Watanzania wenzenu, kwa sababu tu ya husuda, wivu, ubinafsi, roho ya chuki, na tamaa ya 10%
 
Kama kesi Iko mahakamani hamna shida, wasiwasi wangu huenda songoro marine na huyo Basiga walikubaliana ili baadae apate chochote lakini baadae wakadhulumiana hiyo ndiyo michezo ya wabongo.

Kumbuka songoro marine ndio wametengeneza vivuko vya Azam tax
 
Je, ukiondoa hilo suala la wahandisi! Vivuko na Meli zote walizotengeneza zina shida gani mpaka sasa?

Maana isije ikawa hawajotoa 10% na hivyo mkaona muwasagie kunguni. Wabongo wengi uzalendo 0! Mko radhi muwape wageni hizo zabuni za kujenga vivuko, kuliko kuwapa Watanzania wenzenu, kwa sababu tu ya husuda, wivu, ubinafsi, roho ya chuki, na tamaa ya 10%
Soma uelewe mkuu hakuna kusagiana kunguni, jamaa alikuwa mfanyakazi wa Songoro marine akaacha kazi, ila kampuni ya Songoro ikaendelea kutumia documents zake kuomba zabuni maeneo mengi tu, jamaa akafahamu akamueleza Songoro akakiri kosa lake, PPRA nao wamekiri hilo jambo.
 
Back
Top Bottom