LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 18,037
- 33,681
Kwa miaka nenda miaka rudi maelfu ya watafiti duniani wamekuwa wakiutafuta " ufunguo " halisi wa mfalme suleiman..
Kwamba mfalme alifanyaje hadi kuwa na nguvu kubwa kiasi kile..
Moja kati ya sifa alizokuwa nazo mfalme Suleimani ni kwamba alikuwa anawatawala binadamu na majini wote ( wazuri kwa wabaya)
Majaribio mengi yamefanyika kujua siri ya ufunguo wa mfalme Suleiman. Mfano ; Vimeandikwa vitabu mbalimbali vikidaiwa kwamba ni maandiko ya mfalme Suleimani mwenyewe. Moja kati ya vitabu hivyo ni pamoja na kile kinacho wazungumzia wafalme 72 wa kijini ambao wote wali surrender kwa mfalme Suleiman pamoja na kitabu kingine cha siri sana ambacho ndani yake mfalme Suleiman ameandika Elimu ya majini(sio elimu kuhusu majini. Kuna tofauti kubwa sana kati ya elimu ya majini na elimu kuhusu majini. Watu wengi leo hii wanaotajwa kuwa na elimu ya majini, hawana elimu ya majini isipokuwa wana elimu kuhusu majini)
Katika Mafundisho ya siri ya mfalme Suleiman yahusuyo Elimu ya majini imeandikwa kwamba hadi kesho,jina la Suleiman Bin Daud lina nguvu juu ya majini wote. Lina nguvu juu ya falme na mamlaka zote za kijini. Kitabu hicho kianelezea namna ya kuwaamrisha majini kwa kutumia jina la Suleiman Bin Daud. Kitabu hicho kinaelezea kwamba miongoni mwa wana wa Adam hakuna jina ambalo majini wanaliogopa,wanalitii na kuliheshimu kama jina la Suleiman Bin Daud....
Pamoja na yote hayo, mpaka leo hii hakuna mwanadamu aliye fanikiwa kuujua ufunguo wa mfalme Suleiman.
Kama na wewe upo kwenye kundi la watu wanao utafuta ufunguo wa Mfalme Suleiman basi wala usihangaike. Suleiman mwenyewe aliutaja ufunguo huo kupitia kitabu cha Mhubiri 10:19.
Kwenye andiko hilo, mfalme Suleiman anasema " Pesa huleta majawabu ya kila kitu".
Pesa ndio ufunguo wa mfalme Suleiman...
Tafuta hela.