Huu hapa ukweli kuhusu majini (eneo ambalo wanapatikana kwa wingi jijini Dar es Salaam)

Mkuu umesema point muhimu sana, kuamini Mungu na kuamini majini vyote ni imani katika supernatural powers.

Tena, kwa wanaoamini Uislamu/Ukristo ndiyo kabisa, imani za uchawi zimeelezewa mpaka kwenye vitabu.

Mimi nakataa kuwepo kwa Mungu, supernatural powers na pia nakataa kwamba hivi vitabu ni vitabu vitakatifu visivyo na makosa, hivyo, kwa msingi huo, ni rahisi sana kukataa uchawi na majini.

Watu wengi wanaamini mambo ya uchawi na majini kwa kufuatisha vitabu hivi.

Kwa hivyo, kuamini Mungu na dini kama Ukristo au Uislamu, halafu usiamini uchawi na majini, ni contradiction.

Inatakiwa ama ukatae vyote, ama ukubali vyote.
 
Yaani Kwa kifupi uwe chizi au una akili zako,kama hapo umeamua kuwa chizi kongole sana mkuu
 
Yaani Kwa kifupi uwe chizi au una akili zako,kama hapo umeamua kuwa chizi kongole sana mkuu
Inawezekana mimi nikawa chizi.

Lakini, ikiwa kweli mimi chizi, hilo pia litaonesha Mungu muweza yote, mwenye ujuzi wote na mapenzi yote hayupo.

Maana, kuwepo kwa Mungu huyo hakuko logically compatible na ulimwengu ambao machizi wanaweza kuwepo.

Hivyo, ikiwa mimi ni chizi kweli kama unavyosema, hilo nalo linaonesha Mungu huyo hayupo.
 
Huyu mkuu LIKUD hajaendelea kutupa madini mpaka sasa!!? Huu ni unyanyasaji kabisa haoni huruma watu tunajazana humu tunapigana vikumbo yeye katulia tu
 
I like your zeal,keep it up,until the end of your time.Bg up sana mkuu.l
 
Kama mtu hatojua majini, mashetani na hila mbaya huko kanisani ama msikitini wanaenda kumuomba Mungu awaepushe na vitu gani wasivyo vijua!!?
 
Mkuu endelea kutupa elimu wanaojua mambo haya hawataki tusiojua tujue ndio maana wanakua na comment za kukukatisha lengo lako elimu hii uitoayo ni kubwa inatusaidia sana ambao hatuna macho kama yenu nakuomba uendelee na darasa lako mtu mwenye comment ya kukupinga Achana nae we jibu comment za wa hitaji wa kujua ABC
 
Ukisoma elimu ya wanyama ambayo Mfalme Suleiman alijifunza na kuimaster utaweza kujua maana za sauti zinazo tolewa na wanyama mbalimbali.
Elimu ya Wanyama Mfalme Suleiman alijifunza wapi ?

Kuna vitu naona unachanganya hapa.
 
Ukiwa nuruni haya yote hayana madhara kwako. Ufalme wa giza haiwezi nuru.
 
Ukiwauliza tangible evidence ya uwepo wa muumba muweza wa yote wanaishia kukutisha!....hehehe....Mara wakuletee vifungu vya biblia au Qur'an
 
Lakini huyu Muumba lazima yupo tu,kumbuka sisi viumbe wote ni finite,Wakati huyu Muumba ni infinite.
Tunazo njia mbalimbali za kufuata na kuelekea kwake au kujitegemeza kwake.
Jambo Lile Lile tunaona tofauti hata kama wote tunatazama mahala palepale,wengine watasema Ile ni nyekundu na mwingine ataona ni damu ya Mzee,mwingine atasema hiyo ni hudhurungi,na mwingine ataona nyeusi na mwingine haoni chochote Kabisa.
Wanaoamini Muumba yupo wanaamini hivyo na wasioamini wanaamini hivyo,kwa msingi huo hata fikra zinajengeka tofauti Kabisa,ndio maana tunaona tofauti Kwa jambo Lile Lile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…