Huu mchezo wa wafanyabiashara wa k/koo kutoa risiti zenye bei tofauti na iliyolipwa umezidi sasa

TRA wamekaa tu maofisini.
Kazi yao kuzunguka na minyororo na makufuli tu.

Hii michezo wangetakiwa wawe wameshaisthika mapema sana.
Tatizo wakipata nyeti kama hizi watazuga na "inspection" ya wiki mbili then wanarudi kukaa maofisini.
Mie yalinikuta pale Rwegasore duka la mama mmoja hivi Mwarabu karibia Bazaaaaa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Unataka waandike 30000 walale njaaa
Aisee naona TRA wanazungukwa sana, nilipoenda kijijini huko hata ununue kitu cha bei gani hupati risiti. Juzi kati nilinunua vifaa vya ujenzi wa choo, nilichukua cement, sink , bomba, waya mesh, nondo jumla ilikuwa kama 160,000 sikupewa risiti wala nini zaidi ya AHSANTE
 
Ndo maisha mkuu...umepata huduma sepa tu
 
WANATAKIWA KUANZA NA WEWE AMBAYE UMESHIRIKI KUIBA USHURU WA SERIKALI KWA KUKUBALI RISITI YA BEI NDOGO KULIKO BEI HALISI....
 
Mimi nina sura mbaya nini?, maana kabla ya kununua huwa nauliza tena kwa unyenyekevu "risiti inapatikana?" Basi tukimaliza muamala napewa risiti yangu kamili bila nong'ona nong'ona hiyo!

Otherwise wewe utakuwa unataka kupunguziwa bei inayotia hasara, mpka inayotishia kuua biashara ya mtu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
WANATAKIWA KUANZA NA WEWE AMBAYE UMESHIRIKI KUIBA USHURU WA SERIKALI KWA KUKUBALI RISITI YA BEI NDOGO KULIKO BEI HALISI....
 
Mimi huwa nawakubalia maana wanatafuta kipato ila sharti langu huwa na bei ipungue kidogo hapo hata kama ni kitu cha laki tatu wakiandika hamsini sina neno.
 
Sawa tumejua una fridge la laki 8 na 80 na kabati la nguo la laki 3 na 60.
Sasa we unadhani ningeelezeaje mkuu kuhusu manunuzi hayo nawizi unaotumika acha kukalili mkuu afu mi sinaga show off kama unavyodhani nimjinga tu ndio aweza fikiri ni show off Cc: mawazo yakimasikini
 
Kweli kabisa mi mwenyewe baada yakupewa mzigo na risiti hiyo nikawa nawaza hapa nikisimamishwa itakuwajee???? Mana TRA sio watu wakubezaa oooooh!!!!!
 
Kwa hiyoo Kuliko kumfaidisha maskini mwenzakoo wewe unataka Maskini mwenzako azidi kuumia... Afuu mkulu azidi kuneemeka..! Kujikuta mzalendo kumbe kichwani zero...
Boss Wafanya biashara wameshaiba sana sasa niwakati wa kujenga reli, hospital, visima vya maji, elimu Bure, madawa, umeme vijijini n.k lazima tulipe Kodi kwa maendeleo ya taifa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Me nilipewa risiti ya tarehe nyingene kabisaa...! Afu nayo nikaipoteza...
Mi ningewafata tena[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Sasa we unadhani ningeelezeaje mkuu kuhusu manunuzi hayo nawizi unaotumika acha kukalili mkuu afu mi sinaga show off kama unavyodhani nimjinga tu ndio aweza fikiri ni show off Cc: mawazo yakimasikini
ungeweza kusema bila kutaja hizo bei.

Ungeweza kuweka bei za mfano tu, mbona hujataja jina la duka? Mbona hujataja brand za hizo bidhqa ulizonunua?

Kwakuwa unajua wabongo wengi hatuna kabati za nguo na vi fridge vyetu vya laki mbili ukaona utuchokonoe tu kwa hizo bei.

Anyways mkuu usichukulie sana serious hizi comments za mtandaoni wengine tulishachafukwa na roho tokea Oktoba Twentififtini.
 
Acha wivu,nchi ishaharibiwa hii usijifanye mwema sana
 
Wengine hawanong'onezi 360000 inaandikwa 36000/= halafu anakupa huku anakupiga maneno kibaao ww unakunja unatembea
Hahhahhaa daaah laki 360000/= inakatwa zero inapigwa 36000/= daaah wahuni sana hawa
 
Mie nilinunua vyuma vya kuwekea mapazia vyenye thamani ya Tshs360,000/=. Nikapewa risiti sikuangalia nikaweka tu kwenye pochi, nilivyofika home kuangalia nimeandikiwa Tshs6,000/= halafu hata hawakuandika nilichonunua!
Yani wewe walikupiga ndefuu afu kumbe hiyo ndio inakuwa bonus yao serikali inakosa mapato
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…