Huu mchezo wa wafanyabiashara wa k/koo kutoa risiti zenye bei tofauti na iliyolipwa umezidi sasa

Yani wewe walikupiga ndefuu afu kumbe hiyo ndio inakuwa bonus yao serikali inakosa mapato
Siku hizi niko makini lazima niombe risiti, na nikishapewa naisoma kwa undani haswaaaa
 
amatolo! [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
Hao TRA waanze na wewe kwanza ndio wengine wafuate.

Binafsi nikipata nachotaka natembea mbele labda niambiwe kuna msako ndio ntadai risit!

TRA wanatukung'uta makodi makubwa bila kujali hali ya biashara alafu mm ndio nije kuwajali wao?
 
Daaah mkuu bado upo karne nyingi sana za nyuma pole sana sasa kuwa na vijisenti nikuringishia psychologically nimeshakujua nimtu wa type gani na mazingira uliyokulia ila take it simple tuu, by the way nimewlezea kitu real sikutaka bla bla za uwongo mkuu
 
WANATAKIWA KUANZA NA WEWE AMBAYE UMESHIRIKI KUIBA USHURU WA SERIKALI KWA KUKUBALI RISITI YA BEI NDOGO KULIKO BEI HALISI....
Hapana mi nilikuwa makini sana mkuu
 
We utaacha watu wakae katika milango ya kila duka!!
 
Kijana Mwenzetu hiyo ni roho mbaya zaidi ya Nyoka, hivi hata wakikupa hiyo risiti halali na serikali ikapata fedha ya kununulia wabunge, wewe faida yako ni ipi?

Yaani 140,000 walivyokosa kukupa risiti ndio uumie hivyo? Kosa lako sio mfanyabiashara ungejua kwa nn wanafanya hivyo.
 
Chagua iyo risit au wafunge maduka waje nyumbani wako waibe iyo fridge.
nawenyewe wanapata faida humohumo watakula wapi wenzako,kumbuka wana watoto wasome shule nzuri wale vizuri...

Wakikuibia dukani kwao nawenyewe wataenda kuchangia hospital, idara ya maji,tanesco n.k
 
Chamsingi ungeishauri serekali iwafukuze machinga wote na wenyewe wafungue maduka maana haiwezekani wengine wawe na msamaha wa Kodi kwa asilimia 100 , wengine wawe wanalipa wakati wengine hawalipi wakati wote mnauza Kama kawaida, wapo machinga wenye mitaji mikubwa tu ukiangalia vitu walivyomwaga chini ni duka tosha, Sasa c afadhal hao wanaolipa kidogo kuliko hawa wenye mitaji mikubwa pia (machinga wenye maduka waliyoyamwaga chini) lakini hawalipi kabisa
 
Mimi sio mzalendo kwenye kodi. 700,000 ninayokatwa kwenye PAYE inatosha sana.
Unalipa kodi halafu matumizi yanayofabywa kwa maslahi ya mtu mmoja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…