Huu mfumo unachangia upotevu wa mapato na wizi Serikalini

Huu mfumo unachangia upotevu wa mapato na wizi Serikalini

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Tanesco wanazalisha umeme na kuuza kwa taasisi za Serikali. Taasisi za umma zinakusanya pesa na kuziwasilisha hazina moja kwa moja, lakini Tanesco wanakwenda kwenye taasisi za umma kukata umeme kwa sababu wameshindwa kullipa bili huku pesa za kulipa bili zikitoka hazina. Kwa bajeti ya umeme isipelekwe kwa muhifadhi fedha ambaye ni hazina?

Taasisi za uma zinatumia maji na bili isipolipwa wanakatiwa maji huku mkata maji akijua fika kwamba mlipaji ni hazina....kwanini bili za maji zisielekezwe hazina? Kibaya zaidi hata malipo ya maji nayo yanarudi hazina. Kwanini haya madeni yasijioffset yenyewe huko hazina.

TTCl anatoa network kisha anakata asipoliipwa na akilipwa anapeleka fedha hazina ambako aliyemlipa pia anatoa fedha huko huko, kwanini bili zisipelekwe hazina?

Nadhani upo umuhimu wa bajeti za uendeshaji ofisi hasa za umeme, maji, network zisiwekwe kwenye fungu la kila wizara, ziwekwe wizara ya fedha. Taasisi za umma ziwe zinapeleka bills tu na madeni yanajilipa ndani ya hazina bila kukata huduma.

Mfumo huu wa uzungushaji fedha una hasara zifuatazo;
1. Pesa hizi zinapitia makato mengi yasiyo ya lazima ambayo yangetumika kufanyia kazi nyingine. Tukumbuke Sasa hivi hazina wanapokea fedha kwa mfumo wa elekronic hivyo hakuna sababu yakutrasfer cash from one office to another. Fedha itoke hazina,iende wizarani au idarani,ishuke mkoani then kituoni au ofisi za wilaya.

2. Watumishi wasiowaaminifu wamekuwa wakitumia hizi fedha kufanyia Mambo mengine yasiyo na tija ikiwemo kujilipa posho za safari. Bili ya maji hailipwi Wala kupewa kipaombele Bali fedha za kazi hiyo zinapelekwa kwenye safari, mwisho yankuwepo malimbikizo makubwa ya madeni. Kwanini wasikate juu kwa juu?

3. Serikali inapoteza fdedha nyingi pale huduma zinapokatwa kwa taasisi moja kushindwa kulipa bili. Unadaiwa milioni kumi unakatiwa huduma na kusababisha kukosekana kwa mapato au wakati mwingine kutolewa huduma kinyume Cha taratibu nakujenga mianya ya upigaji.

Bili zilipwe kutoka hazina moja kwa moja tuache kutapanya fedha za miradi ya maendeleo
 
Back
Top Bottom