Huu mfumuko wa bei unaoendelea nchini utaliangamiza Taifa kiuchumi na kiusalama

Huu mfumuko wa bei unaoendelea nchini utaliangamiza Taifa kiuchumi na kiusalama

Kwa sasa kila kitu kimepanda sana. Hali ya maisha inazidi kuwa mbaya. Baada ya mwaka mmoja, kama hali itaendelea kuwa hivi, uchumi wetu utaanguka.

Hali mbaya ya kiusalama inayochochewa na uchumi ulioanguka kutokana na mfumuko wa bei itakuwa dhahiri.

Serikali na Taasisi zake, kwa bahati mbaya sana, wameshindwa kudhibiti hali hii.
Acha uchumi uanguke tu sisi tuko busy kubambikia kesi za ugaidi wapinzani
 
Tuache malalamiko maana tunaishi kwenye dunia ambayo kujenga makazi ni jambo la msingi na kumiliki gari ni anasa... Huu ni mwanzo tu, tutafika hata kama tutaikaribia Zimbabwe ila Chips-Yai haijapanda bei.
 
Dunia nzima bidhaa zote muhim ndani ya miezi hii minne kila siku zinapanda kutokana na harakati za kiuchumi kufunguka kwa kasi baada ya kifungo cha COVID, angalia bei ya mafuta ghafi , Steel, gas, copper, mahitaji yameongezeka balaa..
 
Kwa sasa kila kitu kimepanda sana. Hali ya maisha inazidi kuwa mbaya. Baada ya mwaka mmoja, kama hali itaendelea kuwa hivi, uchumi wetu utaanguka.

Hali mbaya ya kiusalama inayochochewa na uchumi ulioanguka kutokana na mfumuko wa bei itakuwa dhahiri.

Serikali na Taasisi zake, kwa bahati mbaya sana, wameshindwa kudhibiti hali hii.
Unajua nini wewe kwenye uchumi? Mfumuko wowote wa bei wa single digit hauna madhara yoyote kwenye uchumi bali unachochea ukuaji wa uchumi na biashara.

Ukiona Tzn kuna Hali mbaya hamia mojawapo Kati ya nchi zifuatazo 👇

Screenshot_20211022-185621.png

Screenshot_20211022-185717.png
 
Kule Mahindi yanakosa wanunuzi huku watu wanalalamika bei kupanda ?

Something is very wrong somewhere....
 
Serikali ipo na pesa za Corona na Mikopo wanaamini hizo pesa zitainua Uchumi
Utasikia TRA wamekusanya zaidi pesa za kujenga Stand ya Arusha wanategemea kwenda Kukopa
 
Wiki ya kwanza nimenunua Nondo tsh 18,000/ wiki iliyofuata 22,500 wiki iliyofuata 25,000
Mafuta ya kula Sundrop lita 10 mwaka huu mwanzoni nilikuwa nanunua 40,000 mwezi wa 5 hadi ni tsh 80,000 ongezeko la hali ya juu sana.!
 
Dah! Aisee vifaa vya ujenzi vimepanda bei ghafla mpaka inaogopesha! Mbaya zaidi hakuna cha Rais, Waziri Mkuu, au Waziri mwenye dhamana aliye jitokeza mpaka sasa kutolea tamko.

Hili jambo linasikitisha na kuhuzunisha sana.
Rais aseme wamtii? Ushahau ya mabando?

Na alivyobadili mawaziri ndiyo bei imepandishwa 100%!

Hii nchi hii, tunakoelekea siko!
 
Back
Top Bottom