Huu mgao wa umeme unaendeleaje nchini, why serikali inaficha na kudai kuna ziada ya umeme?

Huu mgao wa umeme unaendeleaje nchini, why serikali inaficha na kudai kuna ziada ya umeme?

Mtafute yule kijana aliyevumbua umeme wake akufanyie mambo "umeme wa kudumu "
 
Tujikumbushe
IMG_20210228_193709_946.jpg
 
Kuna mgao wa umeme unaendelea nchini, lakini wizara ya nishati na serikali kwa ujumla wanaogopa kutangaza, pia wanajinasibu kuwa tuna ziada ya umeme.

Ni vizuri mtutangazie, ili tuwe tunajiandaa mapema, kuliko kukaata bila taarifa. Najua hamuwezi kutangaza kuna mgao japo upo na hii ni kulinda sijui nini.

Nchi yetu wote tusifichane
Achana na watu wa "kiki na misifa!' Hata zile mbwembwe za viwanda kwisha.
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

FEBRUARI 24; 2021

TAARIFA YA MATENGENEZO KATIKA VITUO VYA KUZALISHA UMEME VYA UBUNGO II NA KINYEREZI II

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa matengenezo ya miundombinu ya Umeme katika vituo vya kufua Umeme kwa Gesi Asilia vya Ubungo II na Kinyerezi II yanaendelea.

Kutokana na matengenezo haya, baadhi ya maeneo nchini yataathirika kwa kukosa huduma ya Umeme kwa nyakati tofauti.


Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi kuhakikisha mashine zinatengemaa haraka.

Tutaendelea kutoa taarifa kadili kazi ya matengenezo inavyoendelea.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au kudondoka chini.

Toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu nawe, au wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: - Kitengo cha Miito ya Simu 028 276 2120 na 0783 521070

Mitandao ya Kijamii :
Website:

www.tanesco.co.tz

Instagram: tanescoyetu

Barua pepe: [email protected],

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook: Tanesco Yetu


Imetolewa na;
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO -
MAKAO MAKUU.
 
Serekali inaficha ili isizue taharuki!Tuna serekali inayoogopa wananchi wake kupatwa na taharuki kuliko inavyoogopa wananchi wake kufa ndiyo maana ipo kimya kwenye ishu ya Corona ili kuzuia taharuki.
 
Huku Pugu walikata Jana saa moja hata muda uporudi sijui ni saa ngapi.
Leo tena muda uleule mpaka sasa hivi bado haujarudi
 
Kuna mgao wa umeme unaendelea nchini, lakini wizara ya nishati na serikali kwa ujumla wanaogopa kutangaza, pia wanajinasibu kuwa tuna ziada ya umeme.

Ni vizuri mtutangazie, ili tuwe tunajiandaa mapema, kuliko kukaata bila taarifa. Najua hamuwezi kutangaza kuna mgao japo upo na hii ni kulinda sijui nini.

Nchi yetu wote tusifichane
Kuna watu wameibuka kwa kasi kusema umeme ulikuwa haukatiki awamu ya 5 [emoji852][emoji852][emoji852] hii ilikuwa ni awamu ya ngapi kwani?
 
Back
Top Bottom