Huu mlango wa Emergency wa ndege unaozungumzwa ndio upi wajuzi naomba mnijuze

Huu mlango wa Emergency wa ndege unaozungumzwa ndio upi wajuzi naomba mnijuze

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Kumekuwa na sinto fahamu mitandaoni kila mmoja akiongea lake ikiwemo manusura wa ajali ya ndege iliyotokea mkoani Kagera.

Ni kweli ukisikikiza maoni ya watu kwa makini unaona kuna hoja hapa ya kujadili, je mlango wa Emergency wa ndege ni upi hapa, muokoaji alitumia dhana gani kuufungua? Au aliukuta upo wazi ndipo akatimiza jukumu lake la uokozi?🤔🤔



7CD7FB12-6A8D-430E-86B4-C2BD73076513.jpeg
 
Kusikia ‘mlango wa nyuma’ kuna watu wamewaza mbali na wameelewa tofauti sana, muwe mnafafanua tafadhali.
 
Watu wana gubu, dogo kafungua mlango yeye ndio anajua kafunguaje. Ila sasa hivi kila mtu anajifanya expert wa milango ya ndege. Mwanzoni kuna mtu alikuja na nadharia kua dogo kufungua mlango ndio kulisababisha maji kuingia ndani! Mwacheni dogo ale faida za alichofanya hizi nyingine ni wivu tu na ujuha kuendelea kujadili yaliyopita.

Mnachotakiwa kujadili ni kwa nini mamlaka husika zinazembea na kutumika kwa dogo kuzima uzembe wa serikali katika uokoaji.
 
Back
Top Bottom