Huu mpira wa Simba una boa!

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Mimi ni shabiki wa Simba,ila aina ya uchezaji wa Simba kwa dunia ya sasa unaweza kufungwa hata na timu ya umitashumta.

Mchezo upo slow,skills duni,na kushindwa kujituma ipasavyo.

Kuna timu tunashabikia ulaya inafungwa ila unatoka bado una imani nayo kwa kuwa unaona bahati tu haikuwa yao.

Mpira wa sasa unatakiwa kuwa na kasi nguvu na akili.Acheni kujidai mnacheza eti show game wakati hata uwezo wenyewe hamnao.

Hawa wanaosajili wanapaswa kuangaliwa sana kwani naona sasa huenda kweli ni wapiga dili.Hawasajili wachezaji wa uhakika.Kwani kama mnalipa mabilioni kwa mwaka mmoja tu kwa kikosi hiki,inatia shaka iwapo kweli mpo serious

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumejaribu kuzima ila bado police wabishi,saizi tunapiga namba ya Hans Mabena (refa),bado iko busy......ngoja tutume muamala atashtuka
 
Nyie vyura mnajiita ' Mabingwa wa kihistoria ' tulieni basi, kwani na nyie mnalitaka kombe ? Mpaka mtakapolikana hilo jina mnalojiita ndo mtakuwa serious kutafuta 'kombe' .na mtaacha kuleta mapro kama Mo Linga na rafiki yake Ipe.
 
Viongozi kumuondoa Uchebe sawa labda walikuwa na sababu za msingi ambazo sisi wengine hatuzijui lakini je huyu kocha waliyemleta ana uwezo sawa na Uchebe? Au kamzidi ujuzi Uchebe?

Jibu ndio hilo tunaiona Simba sasa inapelekeshwa hata na Polisi, Namungo, Mwadui n.k tena uwanja wa Taifa ambao msimu uliopita kafa hapo Nkana, As Vita, Al Haly na akina Soura.

Viongozi shitukeni chukueni hatua kabla mambo hayajaaribika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…