Huu mradi unanichanganya akili; nisaidieni jamani



Nakushauri chukua majogoo kama kumi hivi kisha yatumbukize kwenye hilo banda...kisha baada ya siku 7 utapata jibu.

Watataga asubuhi, mchana jioni hao...puumbav
 

mkuu biashara gani hiyo!
 
Pamoja na ushauri mzuri kutoka kwa wachangiaji waliotangulia, nami nakushauri ujaribu kuchanganya chakula mwenyewe kama huwa unanunua. Katika mfuko mmoja wa pumba (65kg), weka dagaa 10kg, mashudu ya alizeti 20kg, premix ya kenfeeeder 2kg, chokaa 4kg, mifupa 2kg, chumvi ya unga 0.5 kg, mahindi ya kubaraza 5kg, DCP 0.5 kg. Changanya vizuri mchanganyiko wako.

Hakikisha kuku wako wanapata chakula cha kutosha, banda lina usafi na hewa ya kutosha, kuku wasibanane. Mfano kwa idadi ya kuku wako ukiwa na banda la ukubwa wa 24m[SUP]2[/SUP] itakuwa vizuri.

Pia usikate tamaa mapema kwa vile aina nyingine za kuku wanafikia kiwango cha juu kuanzia miezi sita.
 
Pamoja na majibu mazuri ya Mdizi pia angalia kama wanapata direct sunlight mwanga wa jua unatumika kama catalist ya hicho chakula wanachokula. Mwanga wa jua muhimu! Nawasilisha.
 
Mkuu usikate tamaa kunakitu tunaita kuku kuchanganya ambapo mara nyingi kuku huanza kuchanganya kwa maana ya kuku wengi/wote kuanza kutaga kuanzia miezi sita ikipita miezi sita ndo uanze kuwa na wasi wasi
 
Mkuu usikate tamaa kunakitu tunaita kuku kuchanganya ambapo mara nyingi kuku huanza kuchanganya kwa maana ya kuku wengi/wote kuanza kutaga kuanzia miezi sita ikipita miezi sita ndo uanze kuwa na wasi wasi


Asante sana Sabayi na wengine wote mliochangia na mnaondelea kuchangia mada hii. Nimejifunza mengi hasa ukizingatia mimi bado mchanga kwenye fani hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…