Huu mradi unanichanganya akili; nisaidieni jamani

Huu mradi unanichanganya akili; nisaidieni jamani

Nimefuga kuku 180 wa mayai (kuku wa kisasa). Lakini naona hawatagi mayai ipasavyo. Niliwanunua kuku hawa mwezi wa april tar 15, 2012 wakiwa vifaranga kabisa. Nimehudumia tangu aprili hadi leo september. Nilitegemea niwe napata mayai 150 (tray 5) au zaidi kwa siku. Lakini hadi sasa kuku wanaotaga wapo 75 hadi 80 tu, na nakusanya mayai tray 2 na nusu tu na wameanza kutaga mwezi wa nane. Hii inaashiria kuwa takribani kuku 100 hawatagi. Naomba msaada nifanyaje ili wote wawe wanataga mayai kama nilivyotegemea?


Nakushauri chukua majogoo kama kumi hivi kisha yatumbukize kwenye hilo banda...kisha baada ya siku 7 utapata jibu.

Watataga asubuhi, mchana jioni hao...puumbav
 
Hizi biashara nyingine una risk tu....inakua kama kamali anytime unawin au unapoteza mazima....umetumia mtaji mkubwa alaf return yake ya kubahatisha....kwanini usifanye biashara iliyo na minimum risks at the same time return ni kubwa !! ona sasa pesa inavyopotea....mimi kuna biashara nafanya ina risk ndogo sana....na hata kama sijauza kitu....sina cha kupoteza na kama nikiuza faida napata tena kubwa tu...ila still mtaji niliouweka ni mdogo sana !! Cha muhimu ni kujituma kwako tu. Ni PM kwa habari zaidi....

mkuu biashara gani hiyo!
 
Pamoja na ushauri mzuri kutoka kwa wachangiaji waliotangulia, nami nakushauri ujaribu kuchanganya chakula mwenyewe kama huwa unanunua. Katika mfuko mmoja wa pumba (65kg), weka dagaa 10kg, mashudu ya alizeti 20kg, premix ya kenfeeeder 2kg, chokaa 4kg, mifupa 2kg, chumvi ya unga 0.5 kg, mahindi ya kubaraza 5kg, DCP 0.5 kg. Changanya vizuri mchanganyiko wako.

Hakikisha kuku wako wanapata chakula cha kutosha, banda lina usafi na hewa ya kutosha, kuku wasibanane. Mfano kwa idadi ya kuku wako ukiwa na banda la ukubwa wa 24m[SUP]2[/SUP] itakuwa vizuri.

Pia usikate tamaa mapema kwa vile aina nyingine za kuku wanafikia kiwango cha juu kuanzia miezi sita.
 
mkuu Kig

nina wasiwasi na feeding management ... nikiwa nina maana ya kwamba inawezekana kuku (layers) hawakulishwa evenly .. yaani kuna kuku hawakupata chukula cha kutosha kulingana na feed program (grams of feed per day per each lay hen) ... hii inatokana na upungufu wa vyombo vya chakula bandani (feeders) na kupelekea kuku wengine kuwa na lishe isiyotosha (insufficient feed) .... hii inawafanya kuku waliokosa hii lishe pia kukosa virutubisho na wadini yatakayowafanya watage.... virutubisho hivi ni kama vile lycen na DCP ..... pia sababu nyingine inawezekana kabisa uliwabania chakula

hivyo basi cha kufanya ... chukua kuku anayetaga na wengine Unadhani hawatagi .... pima uzito wao na ulinganishe .... ukiona kuna tofauti ya uzito wa +/- 0.15 to 0.2kg.... hapo kuna tatizo la required weight to lay egg

nakushauri ufanye sorting ya kuku wasiotaga na uwauze wasiendelee kula na Kulala bure ili u-replace vifaranga vingine

all the best
Pamoja na majibu mazuri ya Mdizi pia angalia kama wanapata direct sunlight mwanga wa jua unatumika kama catalist ya hicho chakula wanachokula. Mwanga wa jua muhimu! Nawasilisha.
 
Mkuu usikate tamaa kunakitu tunaita kuku kuchanganya ambapo mara nyingi kuku huanza kuchanganya kwa maana ya kuku wengi/wote kuanza kutaga kuanzia miezi sita ikipita miezi sita ndo uanze kuwa na wasi wasi
 
Mkuu usikate tamaa kunakitu tunaita kuku kuchanganya ambapo mara nyingi kuku huanza kuchanganya kwa maana ya kuku wengi/wote kuanza kutaga kuanzia miezi sita ikipita miezi sita ndo uanze kuwa na wasi wasi


Asante sana Sabayi na wengine wote mliochangia na mnaondelea kuchangia mada hii. Nimejifunza mengi hasa ukizingatia mimi bado mchanga kwenye fani hii
 
Back
Top Bottom