Huu mwaka kweli wangu, maana majanga hayaishi

Huu mwaka kweli wangu, maana majanga hayaishi

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
Wakuu, siku ya leo haikuwa mbaya sana. Wote tuliamka salama na baada ya wife kunichemshia maji ya kuoga kwenye kuni basi akawa pale uwani anafua vikanga vya mkojo alivyo tumia usiku uliopita.
Baada ya kunitia viungo kwenye maji ya kuoga, basi nika karibishwa nikaoge kama kawaida.
Mzee kama kawaida nikajifunga msuli na nikachukuwa mswaki wangu wa mti, huyoooo nikatoka nje ili nikakoge.

Nilipo toka nje pale uwani palikuwa na wamama kama wenne wengine wapangaji wenzetu, walikuwa wanafanya kazi za hapa na pale, kama kawaida nikawasabahi na kisha nikamchukuwa mtoto wetu mdogo aliekuwa anacheza pembeni ya mama yake na nikawa kidogo nacheza nae huku nikimrusha juu na tukifurahi kwa pamoja.

Lahaula....Mara paap, msuli ukadondoka chini na wakati huo mtoto alikuwa hewani nimemrusha juu. Wakuu hapa kidogo nilichanganyikiwa maana wale wamama nao walianza kupiga kelele na wengine wakakimbilia ndani na mmoja yeye naona alisimama na akawa ananiangalia zaidi kuanzia maeneo ya kiunoni kushuka chini.

Baada ya kelele ile, ndipo wife akakimbia chap kuja kuniokotea msuli na kunihifadhi wallah.
Dahhh.....

Leo nimeaibika sana, ingawa kuna huyu mama mpangaji mwenzetu ambae alikomaa kunitizama saizi naona kila tukikutana anatabasamu tu, sasa sijui bado ananicheka ama ananifurahia...!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu, siku ya leo haikuwa mbaya sana. Wote tuliamka salama na baada ya wife kunichemshia maji ya kuoga kwenye kuni basi akawa pale uwani anafua vikanga vya mkojo alivyo tumia usiku uliopita.
Baada ya kunitia viungo kwenye maji ya kuoga, basi nika karibishwa nikaoge kama kawaida.
Mzee kama kawaida nikajifunga msuli na nikachukuwa mswaki wangu wa mti, huyoooo nikatoka nje ili nikakoge. Nilipo toka nje pale uwani palikuwa na wamama kama wenne wengine wapangaji wenzetu, walikuwa wanafanya kazi za hapa na pale, kama kawaida nikawasabahi na kisha nikamchukuwa mtoto wetu mdogo aliekuwa anacheza pembeni ya mama yake na nikawa kidogo nacheza nae huku nikimrusha juu na tukifurahi kwa pamoja.
Lahaula....
Mara paap, msuli ukadondoka chini na wakati huo mtoto alikuwa hewani nimemrusha juu. Wakuu hapa kidogo nilichanganyikiwa maana wale wamama nao walianza kupiga kelele na wengine wakakimbilia ndani na mmoja yeye naona alisimama na akawa ananiangalia zaidi kuanzia maeneo ya kiunoni kushuka chini.
Baada ya kelele ile, ndipo wife akakimbia chap kuja kuniokotea msuli na kunihifadhi wallah.
Dahhh.....
Leo nimeaibika sana, ingawa kuna huyu mama mpangaji mwenzetu ambae alikomaa kunitizama saizi naona kila tukikutana anatabasamu tu, sasa sijui bado ananicheka ama ananifurahia...!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha yakiwa magumu kila mtu anajikuta mchekeshaji
 
Kuna mpuuzi angedaka msuli alafu mtoto atajua mwenyewe uko juu
 
Back
Top Bottom