Huu mwendo, bado kuna utaratibu wa ving'amuzi vya mabasi?

Huu mwendo, bado kuna utaratibu wa ving'amuzi vya mabasi?

sijaelewa

Senior Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
101
Reaction score
56
Habari wanaJF nipo safarini ndani ya basi fulani ya Njombe,

Mmmmhh huo mwendo, unanipa mashaka kama bado kuna utaratibu wa ving'amuzi maana huwa vinalia kila dereva akifika spidi 80 kwa saa.

Kwenye hili basi hakuna hata kubeep, mara kutaka kumpita basi mwenzake mara break za ghafla. Nisaidieni kujua hivi utaratibu wa ving'amuzi bado upo kweri?
 
mkuu tunaelekea uchaguzi, omba tuu Mungu usafiri salama mambo mengine yaache tuu. unadhani wahusika hawajui?
 
Si umwambie dereva apunguze mwendo maana wewe ndo uko kwenye hilo basi. kama umeshinda kumwambia mimi sioni haja ya wewe kuja kuanzisha uzi unalalama, labda una haja kubwa😃😃 subiri tu dereva atasimamisha bas uchimbe dawa.
 
Download app ya speedometer kisha ifungue,itakua inasoma speed ya basi ulilopanda kisha tuletee screenshot hapa.
 
Si umwambie dereva apunguze mwendo maana wewe ndo uko kwenye hilo bas. kama umeshinda kumwambia mimi sioni haja ya wewe kuja kuanzisha uzi unalalama, labda una haja kubwa[emoji2][emoji2] subiri tu dereva atasimamisha bas uchimbe dawa.
Kuna dereva wengine huwa ni wabishi, pia hata baadhi ya abiria wapo ambao hushabikia mwendo kasi wa hatari ili wawahi kufika.
 
Tutajie Bus Gani Hilo
Acha Kupoteza Muda Wakati Dereva Mpo Naye Unashindwa Hata Kusema
Kila Bus Lina Number Za Police & LATRA
Hapo Mbele, Kachukue Upige Tena Ni Bure
 
Pamoja na majibu yaliyotolewa na wadau hapo juu ulichokileta kina mantiki, na zaidi ukiacha Hilo basi unalosafiria binafsi huwa nashangaa sana mabasi yanavyopita kwenye alama za 50, gari nyingine hupunguza mwendo lakini mabasi mengi huwa hayapunguzi mwendo na hupita na zaidi ya 50. Wale wanaokaa kwenye hizo 50 na kupiga picha wanaopita na zaidi ya 50 huwa hawapigi picha mabasi. Mara nyingi gari nyingine ambazo hupita na zaidi ya 50 ndio hupigwa picha na kukamatwa mbele.
Hapa sijui inakuwaje.
 
Back
Top Bottom