Mkuu Kishina cha Mshahara,
Salary Slip , kwanza asante kwa uzi huu, pili naheshimu mawazo yako, mwisho naomba kutofautiana na wewe, hoja yako hii sio kweli !.
- Mungu huweka tawala zote za mataifa na tawala hizo zinaongozwa na watu.
- Dhambi au maovu yoyote hayajitendi yenyewe, yanatendwa na watu, hivyo sii kweli kuwa uovu au dhambi ndio unaongoza nchi na sio kiongozi.
- Kuna baadhi ya dhambi au uovu ambao kwa macho ya kibinaadamu ndio tunaona kama dhambi au ni uovu, kumbe ni mpango wa Mungu mwenyewe ameruhusu dhambi hiyo au uovu huo utendeke ili baadae autumie kudhihirisha ukuu wa Mungu, hivyo mtenda dhambi huyo au mtenda uovu huo ataendelea kubarikiwa kwasababu huo ndio mpango wa Mungu.
- Na iwapo dhambi hiyo au uovu huo sio mpango wa Mungu, then ni Mungu mwenyewe ndio hutoa hukumu kwa kila mtenda dhambi au mtenda uovu na sio kweli dhambi au uovu ndio huongoza.
- Na sasa nimalizie hapa kwa faida ya wengine, nchi yetu hapa ilipo, tunakwenda vizuri, so far so good, kiongozi aliyepo hajatenda dhambi yoyote, au uovu wowote kustahili hukumu yoyote ya Mungu.
Mungu Ibariki Tanzania.
P