Huu ndio Muda sahihi wa Kujumua vitu kutoka vijijini kama vile Kuku, Ng'ombe, Mbuzi...

Huu ndio Muda sahihi wa Kujumua vitu kutoka vijijini kama vile Kuku, Ng'ombe, Mbuzi...

Myahudi Jr II

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2016
Posts
6,816
Reaction score
8,809
Habari za asubuhi......

Bwanaaaa weeeee, Wasukuma wamebarikiwa sana kwa habari za mkono kinywani tatizo wabahili sanaaaaa, wana mamifugo ya kila aina ila kuchinja ni mwiko mpaka lianguke hapo chini life ndio mtakula nyama.

Wasukuma, wakilima wanapata kweli kweli, wakifuga wanapata kweli kweli iwe mbuzi, nguruwe, sungura, Ng'ombe, kanga ndio usiseme, bata ndio kabisaaa, kuku hata usiulize.

Sasa ni hivi, hawa jamaa wakivuna hawauzi kitu wana kiburi na jeuri sana ya pesaaa yaani kuku anaekuuzia 4,000(mama kuku) akivuna atakuuzia 9,000, Jogoo la Mbegu la 8,000 akivuna atakuuzia 15,000

Nachowapenda hawa jamaaa yaaani wana matumizi mabaya ya pesa, wakivuna watapiga urabu hatari sanaaaaaaa maana pesa yoote ni ya mwanaume

Iko hivi

Unakuta ana heka 10, 4 atalima baba, 4 atalima mama, 2 watalima watoto kila mtu akipata hela kwenye hizo heka ni zake wala asiulizwe anatumiaje.

Sasa bwana, Pesa za mavuno zimeishaaaaa wamebaki WEUPE kama Sufu za Kondoo wa Australia, weupe Peeeeee, kila kitu kimeshuka beii

Kuki hadi 3,000 unachukua, Mbuzi aliekua anauzwa 60,000 mwezi wa 5 sasa hivi 30,000 unachukua, Ng'ombe wa 200,000 ukienda Mjini watakuuzia 600,000(mnielewe).

Kwa Wafanya biashara za mifugo, Usiende kutafuta mifugo kipindi cha (April to June)

Tafuta kuanzia (July to December)

July watauza kila kitu ili wapeleke watoto shuleni(haya majamaa bwana yani hela yao ni ina matumizi muda huo hela inapopatikana, kama kuna tatizo anajua atauza kitu anasolve tatizo)

Agust na september watauza wapate pesa za kukodi mashamba

October hadi December watauza ili walime,wanunue mbegu, wapande, wapalilie

January to March watauza mazao ili waliyolima wanapovuna pale wanauza ili wapate pesa ya kununua magunia, madawa ya kuhifadhi, usafiri ndio maana watu wanakimbikiaga maporini kipindi hiki.

Kazi yangu Kuwasilisha.
 
Niletee
  • Mbuzi 100@25,000= 2,500,000
  • Kuku 500@ 3,000= 1,500,000
  • Ng'ombe 50@200,000= 10,000,000
Nifanye biashara ya nyama mkuu
 
Niletee
  • Mbuzi 100@25,000= 2,500,000
  • Kuku 500@ 3,000= 1,500,000
  • Ng'ombe 50@200,000= 10,000,000
Nifanye biashara ya nyama mkuu

Huwezi kununu huku kwa hizo bei halafu ukauziwa kwa bei hizo hizo, hiyo itakua biashara kichaa ndugu

Ndio maana sasahivi utaina milori imepakia matenga ya kuku huko utauziwa 7,000 to 8,000 mama kuku na 15 Lijogoo tena hana hasara kwa bei ya Dsm
 
Back
Top Bottom