Huu ndio ukweli; ajira zipo ila Serikali haina pesa za kuajiri

Huu ndio ukweli; ajira zipo ila Serikali haina pesa za kuajiri

Kwakuwa JK yuko jikoni, ngoja tuanze kutembeza bbakuli tena.ajira zitarudi kama zamani.
 
Ni sawa tuu, lawama si mzigo
Sidhani ila kuwalipsha ada tena ni sawaa lkn itaumiza wazaz hasa wanaoish mazngra ya vijijin huwa ni mtihan mkubwa ktk masual ya elimu tena ukirudsh ada siutafanya watt wakae nyumban waanze kufany mishe nyingne ambaz ni kinyumbe na sheria za nchi kiongoz??
 
Posho na mishahara ya wabunge ipunguzwe na ilipiwe kodi...

Wabunge wasio na uwakilishi kina mdee wanatumia kodi bure tu watoke bungeni, hizo pesa zifanyie maendeleo
 
Mbona kika mwaka maelfu ya wafanyakazi wanastaafu lakini hawataki kuajiri ikiwa ni pamoja na mapengo ya walioondolewa kwa vyeti fake.
Huu ndio ukweli ajira zipo ila serikali haina pesa za kuajiri na kulipa mishahara.

Je, tufanyeje ili kupata fedha za kuajiri na kulipa mishahara?

Nini maoni yako katika hili.

Wewe ungekua ndio kiongozi ungefanyeje ili kupata fedha za kuajiri na kuwalipa mishahara hao ambao utawaajiri?
 
Huu ndio ukweli ajira zipo ila serikali haina pesa za kuajiri na kulipa mishahara.

Je tufanyeje ili kupata fedha za kuajiri na kulipa mishahara?

Nini maoni yako katika hili.

Wewe ungekua ndio kiongozi ungefanyeje ili kupata fedha za kuajiri na kuwalipa mishahara hao ambao utawaajiri?
WANAOLIPWA MISHAHARA YA MILIONI 4 HADI 12 KWA MWEZI WAPUNGUZIWE MISHAHARA HADI KUFIKIA LAKI 8 HADI MILIONI 2 KWA MWEZI ILI NA WENGINE WAAJIRIWE.

WATU WAFANYE KAZI KWA SHIFT YA KILA BAADA YA MASAA 3, ILI WENGI WAINGIE KWENYE AJIRA. (HAPA LAZMA KAZI ZITAFANYWA KWA UFANISI BADALA YA MTU MMOJA KUFANYA KAZI ASUBUHI MPAKA JIONI) NA BAADA YA MASAA 3 KILA MMOJA AKAENDELEE NA MAMBO NA MIPANGO YAKE.

KILA MMOJA ATAKAYE PEWA KAZI APANGIWE KWENYE MKOA WAKE ILI KUEPUSHA GHARAMA MBALIMBALI.

MISHAHARA ISHEPIWE NA KUWEKWA KTK STANDADI NZR AMBAYO SERIKALI ITAMUDU KUWALIPA WAAJIRIWA WOTE.

KUPANGA NI KUCHAGUA, HAKUNA KISICHOWEZEKANA CHINI YA JUA. RAIS AKALIONE HILI.
 
Watanzania mko wapi leteni mawazo yenu hapa badala ya kulaumu viongozi. Tunahitaji mawazo yako kama yapo.
 
Watoe fursa kwa wawekezaji na wapewe masharti mepesi kwenye kuwekeza ili waajiri vijana.., serikali peke yake haiwezi kuajiri wote.
 
Watanzania mko wapi leteni mawazo yenu hapa badala ya kulaumu viongozi. Tunahitaji mawazo yako kama yapo.
Kama hakuna uzalishaji hakuna pesa itapatikana ya kuajiri..

Kuna watu huwa wanasema eti degree zimetosha kitu ambacho si kweli, uhitaji wa wataalam kwenye sekta mbalimbali bado ni mkubwa sana.

Nchi bado ina uchumi mdogo ila cha ajabu vipaumbele tumeweka kwenye mambo yasiyo na tija. Kifupi bado hakuna viongozi wanaowaza kutukwamua toka hapa tulipo.

Ukiangalia hakuna miradi yeyote ya maana inayoanzishwa ya kuweza kutoa ajira, kama bandari ya Bagamoyo tu ambao ni mradi mkubwa sana ambao kwa namna moja au nyingine ungeleta ajira za kutosha, bado viongozi hao hao wakaupiga vita.
 
Warudishe tu ada shuleni ...

Elimu bure ilikuwa mihemko ya kisiasa ,imesababisha serikali inalemewa mpaka haiewezi kuajiti ..

Kudadekiiiiii
 
Nikuulize kuna mahali serikali iliamdikishana mkataba na graduates kua wakimaliza chuo itawaajiri? Kama hakuna mbona unalalamika kama mtoto..nenda kapambane kutafuta pesa..serikali haiwezi ajiri graduates wote mbona hua hamuelewi nyie vichwa maji.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom