Baba Dayana
Senior Member
- Jul 1, 2016
- 144
- 330
Huu ndio utaratibu kwa kumchukua (kamata) mwanajeshi wa JWTZ ambaye anashikiliwa kwenye mahabusu ya Kijeshi iliyo ndani ya Kambi ya Jeshi na kumleta kwenye mahabusu ya muda (temporary custody) ya kiraia.
Askari polisi mkamataji, anatakiwa awe na hati ya ukamataji (arrest warrant) ambayo imetiwa saini na afisa wa polisi mwenye cheo kisicho chini ya Mrakibu wa Polisi (Superintendent of Police (SP)) – kwa faida ya wasomaji, ni cheo kinachofuata baada ya NYOTA TATU (ASP). Pia, saini inaweza kuwa ya afisa mwandamizi wa Kituo husika anachotoka askari huyo (mkamataji).
Hati hiyo ikiwa tayari, askari huyo ataenda mpaka Kambini alipo mtuhumiwa na kumtaka Mkuu wa Kambi, yaani Commanding Officer (CO), kutoa IDHINI kwa kusaini Hati hiyo ya ukamataji. Kama mkamataji ana cheo chini ya ASP, atahitaji 'movement order'.
Hati ya ukamataji ni nyaraka ya KISHERIA, hivyo ni AMRI halali. Kisheria, CO wa Regiment anatakiwa kuitii amri hiyo pasipo kukaidi. Endapo CO atasaini, askari ataruhusiwa kuondoka na mtuhumiwa na kumpeleka kwenye mahabusu ya kiraia ya muda ili kufanyiwa mahojiano na taratibu zingine za upelelezi; ambapo mnaweza kukaa naye kwa muda usiozidi SIKU SABA; japo kwenye suala hili kuna sheria nyingine za nchi za kuzingatiwa.
Kama CO atakataa kusaini ODA ambayo ni AMRI ya mahakama, atakuwa anavunja kifungu cha 114 cha Penal Code; contempt of court!
SUALA LA MUHIMU KUZINGATIA - JURISDICTION.
Mipaka ya kimamlaka ni muhimu kuzingatiwa. Kama eneo la ukamataji liko zaidi ya MAILI 20 kutoka kwa Hakimu aliyetoa ARREST WARRANT, unatakiwa unapofika eneo la Kambi, baada ya kumkamata mtuhumiwa, umtafute Hakimu mwenye MAMLAKA kwenye eneo hilo ambaye atahakiki hati hiyo kisha kutoa IDHINI ya mtuhumiwa kuhamishwa kwenye mamlaka ya mahakama iliyotoa hati. Hili ni TAKWA la kisheria hivyo muhimu kuzingatiwa.
Maelezo haya yamezingatia Sheria ya Ulinzi wa Taifa (The National Defense Act, No. 24 of 1966); vifungu vya 66, 74(1), (2) & (3); vifungu cha 75 & 82. Pia, 'Code of Service Discipline'; code C.7, C.8 & C.65. Vikisomwa sambamba na Sheria ya 'Minimum Sentence Act, 1963' pamoja na 'Scheduled Offences' ya 1963.
Askari, tulia sijamalizi!
Pia soma vifungu 7, 10 & 122 vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai; yaani CRIMINAL PROCEDURE ACT (CPA). Pasipo kuacha Ibara za 13(1) & 26 za Katiba ya nchi & Sheria za Kimataifa kama vile; The Geneva Conventions, ROE & LOAC.
Kuna miongozo & kumbukumbu za mahakama ya kijeshi (Court Marshall) au Service Tribunals pamoja na mahakama za Kiraia.
ANGALIZO,
Umma unafuatilia hili tukio! Tunachokifanya ni KULINDA Katiba ya nchi. Katiba imepiga marufuku UPENDELEO na IMESISITIZA kuwa watu wote wako SAWA mbele ya macho ya sheria.
Mwanajeshi hana KINGA (immunity) dhidi ya makosa ya jinai. Hivyo, tunasisitiza tunataka kuona watuhumiwa wanakamatwa & msije mkafanya taratibu KIMAZOEA halafu watuhumiwa wakashinda kesi kwa sababu ya UZEMBE wenu. Tunajua hoja za KIUFUNDI zinazotumika kuachia watuhumiwa au wafungwa walio karibu na 'mfumo'.
Kama hitaji la kisheria (ushauri) litahitajika, msisite kunitafuta, nitatoa USHIRIKIANO.
#TLS is watching.
UMMA UNAFUATILIA KILA HATUA.
#OperationOfTheLaw ⚖️