Huu ndio uzoefu wangu kwenye Loan allocation na chuo

Omari Issa

Senior Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
168
Reaction score
45
Nimelazmka kufungua uzi huu ili tupeane ufahamu na uzoefu ktk mas'ala ya HESLB loan allocation na Chuo.

Ndg. zangu FIRST YEARS suala la "disbursement" ya mkopo toka HESLB haliangalii "Chuo ulichochagulia" (nitatolea maelezo) isipokuwa inaangalia DEGREE PROGRAMMES uliyochaguliwa nayo, uhitaji wako wa mkopo, hali zako kiuchumi na kijamii.

Kwa mfano wanaweza kusema BED programmes zote vyuo vyote tunawapa 70% (ambayo ni sawa na 500000 kwa mwaka kwa mfano) hii hata ukienda KAMPALA UNIVERSITY ambako ada zao ni xawa na 5,000,000 (kwa mwaka) bado asilimia za bodi zitabaki zilezile. Kwa iyo apa ieleweke wazi tu kuwa mtu yeyote chuo chochote anaweza pangiwa mkopo wowote kulingana na degree program huksika.

Katu usije ukajaribu kuhama chuo pindi jina lako la mkopo limetoka ktk chuo fulani. Hama chuo mara tu majina ya T.C.U yanapotoka kabla hayajapelekwa HESLB.

Usisaini mkopo pindi unapokuja chuoni kwako kisha uka~apply transfer. Utahamishwa na TCU but bodi ni lazma uilipe asilimia zile ulizokula ktk chuo hiko ndpo uhame
 
Tunahitaji watu wa kuelimisha kama ninyi na sio wanaojifanya wanajua kumbe wajinga sana:
 
Naomba kujuzwa, Je ufaulu wa kidato cha sita ni sifa mojawapo ya kupata mkopo?

Kama ndivyo! mwaka huu adi wenye dvsn four tumepata vyuo, Inamaana tusahau kuhusu mkopo?
 
Nijuavyo mimi kwa kukumbuka vigezo walivyoangalia wakati najiunga chuo ni kama ifuatavyo
1. Shule alizosoma muombaji, sio upate mkopo wakati historia yako inaonyesha umesoma feza boys/girls

2. Hali ya uyatima(huna wazazi) hiyo inakua favour
Hali ya uchumi wa familia yako, ndio maana utaulizwa kazi ya baba na kazi ya mama yako.

3. Fani uliyoomba kusoma chuo, hapa kuna fani hazina mkopo kabisa, zingine zina mkopo kidogo na zingine zina 100% unalipiwa, hivyo angalia fani uliyoomba kama ina kipaumbele kwa taifa (priority) ,kwenye guidebook ya TCU

4. Ufaulu wa mtu unaangaliwa ila nadhani ni kiasi kidogo sana.

Kama una sifa 1,2 na 3 nilizozitaja hapo mwanzo hiyo sifa ya 4 ya ufaulu isikupe shida kwa sababu ukishachaguliwa inamaana umepata sifa za kujiunga na chuo hivyo umefaulu ndo maana umechaguliwa.
Kila la kheri mkuu
 
Naomba kujuzwa, Je ufaulu wa kidato cha sita ni sifa mojawapo ya kupata mkopo?

Kama ndivyo! mwaka huu adi wenye dvsn four tumepata vyuo, Inamaana tusahau kuhusu mkopo?
 
Habarini za saiv wanajf?

Mimi nimesoma shule ya kijijini kwa elimu ya o'level ndipo baada ya hapo nkafanikiwa kusoma elimu ya chuo katika level ya Diploma in Civil Engineering.

Tatizo lilijitokeza wakati wa kuapply mkopo ambapo baada ya kuingiza index namba ya o'level ikaniletea information zingine zote isipokuwa jina la shule ilipo niletea (SCHOOL NAME NOT FOUND).

Naulizeni wanaJF je, hiki kinaweza kikawa ni kigezo cha mimi kukosa mkopo? Please naomben mnisaidie.
 
Hakuna kitu kama hcho, kigezo cha wewe kupata mkopo kinategemea na matokeo ya TCU, ukipata shule hata mkopo unaweza ukapata
 
kwa mfano, labda kama unazungumzia grants nikwawaliofaulu vizuri tu according to katiba ya heslb
 
Af we VVU, me stak mfano nataka reality ipoje?

soma maelezo yapo heslb kwa arts upate mkopo wameandika point 4, science , 3 na grants zinatolewa kwa wenye two na one,,,
 
soma maelezo yapo heslb kwa arts upate mkopo wameandika point 4, science , 3 na grants zinatolewa kwa wenye two na one,,,

Inamaana mtu aliepata EES, za PUMP kwa miaka ya nyuma b4 2014.
Alikua hapati mkopo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…