Huu ndiyo Ukubwa wa Simba: Timu 8 zitakazoenda robo fainali CAFCl, zote zinatokea nchi za Kiarabu isipokuwa Simba na Mamelodi

Huu ndiyo Ukubwa wa Simba: Timu 8 zitakazoenda robo fainali CAFCl, zote zinatokea nchi za Kiarabu isipokuwa Simba na Mamelodi

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Wakuu huwa tunaongea kimasihara hapa na kuiponda Simba, kumponda mwekezaji Mo Dewji na kimuita majina ya ajabu.
Screenshot_20230319-081011.png



Screenshot_20230319-081044.png


Wacha-mbuzi uchwara nao utawasikia wakiiponda Simba na kuiita timu ya hovyo.

Lakini kiukweli Simba japo haipo kwenye kiwango chake cha ubora, bado ni timu kubwa sana Afrika, tazama msimamo wa makundi CAFCL.

Club zote zilizo katika nafasi ya kwanza na ya pili zinatoka katika nchi za kiarabu isipokuwa club mbili tu, Simba na Mamelodi Sundows ya Africa Kusini.

Kwa wasiojua soka la Afrika vizuri, mataifa ya Kiarabu ni mtaifa tajiri sana na wachezaji wake hawaendi kucheza ligi za Ulaya kama mataifa ya Afrika Magharibi.
 
Ingekuwa kundi la Simba lina waarabu wawili ndio ingekuwa sahihi kauli yako. Makundi mengine yana timu zaidi ya moja ya kiarabu hivyo unatakiwa kufurukuta ili upate nafasi. Asa kundi lina mwarabu mmoja tu obviously lazima timu anayeungana nae lazima iwe sio mwarabu. Sijui uliwaza nini
 
Waarabu Afrika hii wameyakamata mashindano ya vilabu CAF.

Nimecheki gme ya jana ya Vita na JS Kabylie, Vita alikuwa anaupiga mwingi huku anaongoza goli moja hadi kwenye dkk ya 60 hivi. Waarabu wakawasha moshi uwanja mzima, hata mpira hauonekani. Mpira ulisimama dakika 1 tu ulipoanza tena, Vita bado hawaelewi kinachoendelea jamaa wakasawazisha. Baadae Vita hawajakaa vizuri tena, wakapigwa cha pili.

Jamaa wana michezo michafu sana katika kutafuta ushindi.
 
Ingekuwa kundi la Simba lina waarabu wawili ndio ingekuwa sahihi kauli yako. Makundi mengine yana timu zaidi ya moja ya kiarabu hivyo unatakiwa kufurukuta ili upate nafasi. Asa kundi lina mwarabu mmoja tu obviously lazima timu anayeungana nae lazima iwe sio mwarabu. Sijui uliwaza nini
Anamaanisha kwanini awe Simba na si Horoya AC
 
Katika tafiti zangu, nimegundua Club ya yanga ina-power kubwa sana katika Propaganda za soka Tanzania. Endapo utashindwa kuutazama mpira kwa jicho lako(Independently) basi utafikiri kile wanachotaka ufikiri wao(Yanga), pia utaona kile ambacho wanachotaka uone wao (Young Africans).

Japo, nitakuja na uzi siku moja kuhusu hili, ili nieleze kiundani kabisa, ila hizi ni moja ya sababu zinazowafanya wa-win propaganda za Soka Tanzania.

1. Uwezekezaji katika media: Wamejitahidi sana kuwekeza katika media bora na kwa wachambuzi sahihi(Naomba nisiwataje majina, sina mwanasheria kwa sasa). Ila wengi najua mnawajua.

2. Nature ya Mashabiki wao: Sipendi kum-quote Haji Manara, lakini katika jambo ambalo alikua sahihi, ni hili la mfanano wa akili za mashabiki wa Yanga. Angalia hata hapa JF threads nyingi za mashabiki wa Yanga unaweza sema ni mtu mmoja, ila ID ndiyo tofauti(Kama bado hujaliona hili, chunguza kwa umakini). Wote nia wabishi sana, wanaweza pindisha hata facts. I think wana Mad Love na timu yao.

Mtazamo(Ushindani vs Ukinzani): Ni mara nyingi naona threads za mashabiki wa Simba wakisifia, like Mwananchi ametembeza soka safi leo, Mayele yupo vizuri, Diarra yupo vizuri, Nabi ni kocha wa mpira e.t.c. Ila Yanga ukiona wanasifia kitu Simba basi jua huo ni mtego au hicho kitu hakipo kwa sasa pale msimbazi.
- Konde Boy, Chama, watakuambia ni wachezaji wa kawaida sana.
-Ubora wa Mgunda, walisema ni Jeans yake inatupa matokeo.
-Utampiga Al Ahly yule bora, watakuambia Corona hiyo.
- watapokea wapinzani wa Simba airport.
-Watajaa Uwanjani kushangilia mpinzani wa Simba.

So, Wakati Simba anachukulia kama Yanga ni Mtani/Mshindani wake(Ndani ya ligi). kichwani mwa wana-Yanga wanamuona kama Simba ni MKINZANI wao.

-Best Daddy
 
Katika tafiti zangu, nimegundua Club ya yanga ina-power kubwa sana katika Propaganda za soka Tanzania. Endapo utashindwa kuutazama mpira kwa jicho lako(Independently) basi utafikiri kile wanachotaka ufikiri wao(Yanga), pia utaona kile ambacho wanachotaka uone wao (Young Africans)...
Upo sahihi kabisaa wala hujakosea .Simba wanachukulia utani ila Yanga kwao ni ugomvi/ vita.
 
Anamaanisha kwanini awe Simba na si Horoya AC
Kwani Horoya ni mwarabu? Hata akiwa Horoya bado ni vile vile tu haikuwa vita ya Simba na mwarabu bali itakuwa ni vita ya Simba na ngozi nyeusi mwenzie ambaye ni Vipers na Horoya. labda ingekuwa kuna waarabu wawili ndio alichoongea kingekuwa kina usahihi.
 
Ingekuwa kundi la Simba lina waarabu wawili ndio ingekuwa sahihi kauli yako. Makundi mengine yana timu zaidi ya moja ya kiarabu hivyo unatakiwa kufurukuta ili upate nafasi. Asa kundi lina mwarabu mmoja tu obviously lazima timu anayeungana nae lazima iwe sio mwarabu. Sijui uliwaza nini
Simba haikuwekwa hilo kundi kwa bahati mbaya, iliwekwa kutokana na ranking.

kabla ya kupanga makundi timu za rank ya juu huwekwa pot yake, rank ya inayofuata pot yake, timu za rank ya kati pot yake na rank za mwisho pot yake ili kuepuka timu nzuri zote kuwekwa kundi moja au timu vilaza zote kuwekwa kundi moja.

Simba isingeweza kuwekwa kwenye kundi lenye timu mbili za kiarabu sababu ilikuwa kwenye pot moja na timu nyingi za kiarabu.

Hata hivyo kama hujui, Simba ilishawekwa kwenye makundi na timu za kiarabu na ikazipita, kama umeanza kufuatilia mpira mwaka huu ngoja nikuwekee.

Screenshot_20230312-093434.png

Screenshot_20230312-093608.png
 
Tuache ushabiki maandazi kama baadhi ya wachambuzi wetu wa mpira, kuna mtu wa mpira kabisa alisema shirikisho ni kombe la walioshindwa na leo yupo huko kwa walioshindwa na anashangilia ushindi! Simba wamekua wazoefu sana wa haya mashindano na huo ndio ukweli!
kiukweli hatuna kikosi imara cha kupambana kama miaka 4 iliyopita basi tu uzoefu unatubeba
 
Back
Top Bottom