Katika tafiti zangu, nimegundua Club ya yanga ina-power kubwa sana katika Propaganda za soka Tanzania. Endapo utashindwa kuutazama mpira kwa jicho lako(Independently) basi utafikiri kile wanachotaka ufikiri wao(Yanga), pia utaona kile ambacho wanachotaka uone wao (Young Africans).
Japo, nitakuja na uzi siku moja kuhusu hili, ili nieleze kiundani kabisa, ila hizi ni moja ya sababu zinazowafanya wa-win propaganda za Soka Tanzania.
1. Uwezekezaji katika media: Wamejitahidi sana kuwekeza katika media bora na kwa wachambuzi sahihi(Naomba nisiwataje majina, sina mwanasheria kwa sasa). Ila wengi najua mnawajua.
2. Nature ya Mashabiki wao: Sipendi kum-quote Haji Manara, lakini katika jambo ambalo alikua sahihi, ni hili la mfanano wa akili za mashabiki wa Yanga. Angalia hata hapa JF threads nyingi za mashabiki wa Yanga unaweza sema ni mtu mmoja, ila ID ndiyo tofauti(Kama bado hujaliona hili, chunguza kwa umakini). Wote nia wabishi sana, wanaweza pindisha hata facts. I think wana Mad Love na timu yao.
Mtazamo(Ushindani vs Ukinzani): Ni mara nyingi naona threads za mashabiki wa Simba wakisifia, like Mwananchi ametembeza soka safi leo, Mayele yupo vizuri, Diarra yupo vizuri, Nabi ni kocha wa mpira e.t.c. Ila Yanga ukiona wanasifia kitu Simba basi jua huo ni mtego au hicho kitu hakipo kwa sasa pale msimbazi.
- Konde Boy, Chama, watakuambia ni wachezaji wa kawaida sana.
-Ubora wa Mgunda, walisema ni Jeans yake inatupa matokeo.
-Utampiga Al Ahly yule bora, watakuambia Corona hiyo.
- watapokea wapinzani wa Simba airport.
-Watajaa Uwanjani kushangilia mpinzani wa Simba.
So, Wakati Simba anachukulia kama Yanga ni Mtani/Mshindani wake(Ndani ya ligi). kichwani mwa wana-Yanga wanamuona kama Simba ni MKINZANI wao.
-Best Daddy