Huu ndiyo utofauti wa Kiba na Diamond

ONE 8 inaitwa HANDS ACROSS THE WORLD sio across Africa jitahidi kufanya research kabla ya kuandika insha na hiyo pencil yako ya HB
 
Bado sijaelewa hapo mnaposema Diamond hajui kuimba.
Trey song alikataa kuimba na domo maana hajui kuimba licha ya JK kumpigia chapuo. Neyo hana kiki ndio alikubali kuimba na Learner
 
umenishawishi.
 
umenishawishi.
 
Linex.. Madee..
 
We ndo hujui habari za kiba kabisaaa... Huwezi sema kuwa eti njiwa ndo nyimbo ya kwanza ya kiba.. ! Njiwa utamwachia nani ?[emoji57]
 
Hizi porojo za Daimond hajui kuimba ni propaganda tu,tofauti yake na Kiba katika uimbaji ni sauti na kimsingi sauti haziwezi fanana,Phil Collins,Michael Jackson,Marvin Gaye walikuwa na sauti tofauti za kuimba lakini haimaanishi kuwa kuna mmoja kati yao anajua kuimba kuliko mwingine.Tofauti inapimwa kupitia mafanikio yatokanayo na uimbaji na hii inamaanisha kuwa staili ya uimbaji ya mond imempa mafanikio hayo aliyonayo,kitu pekee cha kufanya ni kumpongeza na kumtumia kama role model kwa wasanii wavivu wasiopenda kujituma ili baadae tuwe na lundo la wanamuziki waliofanikiwa Afrika kama wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo au Nigeria.
 
Kiba anamtegemea mondi kama ray alivyokuwa ana mtegemea kanumba, hatuombei itokee ila siku ikitokea diamond kavuta kiba ndio utakuwa mwisho wa mziki wake.
 
Hizi hadithi za Chibu hajui kuimba mara sijui hana sauti tamu kama fulani mnazitowa wapi?
Mnatumia vigezo gani?

How can u tell ati fulani anajua kuimba kuliko fulani aliefanikiwa zaidi katika huo uimbaji
Mwishowe mtakuja kutuambia mjomba wako huko mwanalumango anajua kuimba kuliko jastini biaba au krisi brown..... Ndiko mnakoelela sasa

Mara ohhh Chibu mfanyabiasha,fulani mwanamuziki,
Wabongo bana hatuwezekaniki kwa blah blah na siasa miingi
 

KUNA vita ya maneno kati ya makundi mawili ya mashabiki wa Muziki wa Bongo Fleva, wanaowashabikia wasanii Alikiba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, kila upande ukidai mtu wao ndiye anajua zaidi kuliko mwingine.

Ni mjadala mpana katika mitandao ya kijamii, mitaani na hata miongoni mwa wasanii wenyewe ambao kwa kificho au waziwazi, wamewahi kuzungumzia nani mkali katika wawili hao ambao wote ni vijana wenye asili ya Kigoma.
Related:NICE PHOTO FROM MSANJA MKANDAMIZAJI WITH HIS WIFE
Alikiba ama King Kiba, ndiye wa kwanza kuingia na kupata jina katika Muziki wa Bongo Fleva, katikati ya miaka ya 2000 akiwa na singo yake ya kwanza, Cinderella ndiyo ilimfungulia milango, kwani alichomoza hadi juu ambako alidumu kwa muda mrefu.

Huenda Diamond amewahi kuimba kwa kuiga baadhi ya nyimbo za Alikiba, kwa sababu yeye alianza kupata jina mwaka 2009, mwaka ambao mwenzake tayari alishakuwa na albamu mtaani.

Unapotaka kufanya ulinganisho wa wawili hawa ni lazima uchague unataka kuwalinganisha nini, vinginevyo unaweza kujikuta umewekeza katika chuki au ushabiki, kitu ambacho hakitakiwi. Kwa mfano, vigumu kupata idadi kamili ya mashabiki wa wasanii hao, ingawa mapokeo ya kazi zao yanaweza kumuongoza mtu kuelewa.

Kitu kimoja cha msingi ambacho wengi wanakubaliana ni kwamba Alikiba ana uwezo mkubwa wa kuimba na mwenye sauti nzuri kuliko Diamond. Msanii mmoja chipukizi, Ibrahim Kidugu ‘Wizzy Rapper’ katika kibao chake cha Kote Nisikike, kwenye mojawapo ya vesi anasema “Ali ni mwanamuziki, Nasibu Mfanyabiashara.”

Maana ya Wizzy Rapper ni kuwa Diamond anafanya biashara ya muziki, ndiyo maana anaonekana kuwa juu ya Alikiba ambaye anafanya muziki kwa mazoea.

Katika ubora wake, Alikiba aliwahi kukutana na mkali wa R&B duniani, R Kelly, katika projekti iliyoitwa One8, ambapo wakali nane wa Afrika walifanya ngoma moja iliyoitwa Hands Across Africa ambao walikuwa ni yeye, Fally Ipupa, 2Face, Amani, Movaizhaleine, 4X4, Navio na JK.

Licha ya Kiba kufika nyumbani kwa R Kelly, studio kwake, alishindwa kutumia ushawishi wa msanii huyo mkubwa ili aweze kumsaidia kuingia katika soko la Marekani. Mbaya zaidi, alishindwa pia kujitangaza kimataifa kupitia Fally Ipupa na 2Face ambao ni maarufu kuliko yeye.
Related:Ugandan singer turns illuminati agent in SA
Ambwene Yessaya ‘AY’ alimkutanisha Diamond na Davido wa Nigeria na akafanya naye Ngoma ya Number One Remix. Hapa kijana yule wa Tandale hakutaka kuishia kwa msanii huyo pekee, akaingia nchini humo na kufanya kazi na wasanii karibu wote wakubwa, wakiwemo waliofanikiwa zaidi, P Square.

Hiyo imempa Diamond kujulikana zaidi na kumfanya kuwa mmoja wa wasanii wakubwa Afrika, kiasi cha wengi kuhitaji kolabo naye kutoka Afrika Kusini, Zimbabwe, Ivory Coast na kwingineko Afrika.

Alikiba haonekani kuwekeza akili yake yote katika muziki anaoufanya. Ni kama mtu ambaye anafanya muziki kwa kujifurahisha na siyo kufikia malengo ambayo mashabiki wake wangependa aende. Ana uwezo mkubwa nyuma ya Mic, lakini ameshindwa kuutumia ili kuliteka soko.

Kiba anaridhika au labda niseme, mvivu. Katika uhalisia ni makosa kumshindanisha na Diamond kwa sababu haoneshi kama ni mshindani wake. Alipokuwa katika ziara yake Ulaya, akaitumia nafasi adimu aliyoipata kukutana na marehemu Papa Wemba na kufanya naye wimbo.

Baada ya kuliweza soko la Afrika, Diamond anaonekana wazi kulitamani la Ulaya na Marekani na hii ndiyo sababu ya yeye kuwa msanii anayelipwa zaidi kuliko wote kwa sasa hapa Bongo.

Kiba hatafuti kolabo na watu wa nje kwa vile anadhani ataonekana anamuiga mwenzake, wakati katika maisha, kuiga vitu vizuri na vya maendeleo ni jambo la kupongezwa.

Hata hivyo, Kiba anayo nafasi ya kubadilika ili aweze kuwa mshindani wa kweli wa Diamond, vinginevyo asahau.

Chanzo:GPL
 
kingine Alikiba HAJUI kuandika mashairi yenye vina kama Diamond.
..nashauri atafute mtu wa kumuondikia coz kuandikiwa sio dhambi.
Yaani wewe ndo hujui anayejua mashairi kabisa au utakuwa hujamwelewa mtoa mada ,Kati ya watu wenye nyimbo zenye mashairi kiba ni mmoja wapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…