DOKEZO Huu ndo uhuni unaofanywa na mitandao ya simu inayouza router za unlimited

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Suluhisho ni ELON MUSK STAR LINK....ambayo wenyenchi wameipiga pini
Wewe unafikiri star link wakati haya makampuni yanayo operate hapa nchni wana hisa nayo.wao ni wajinga wapoteze kula yao Yao ?tusiposhughurika na hao mafisadi hatuwezi kutoboa hata siku.ili mambo yaende sawa ni lazima kuzifuta hizo cartels za wezi.
 
Basi wanatakiwa na wao wauze volume based bundle. Siyo unlimited au time based bundle.
Wanachofanya ni ulaghai na wizi kwa wateja.
Wanachongataza na wanachokupatia tofauti, wanatumia lugha ya ulaghai.
Kuna kampuni iliwahi kupata shida kwa kutangaza maji ya fulani yanatoka kwenye chemichemi iliyopo Kilimanjaro wakati maji hayatoki huko kihalisia.
 
ingekuwa mbele lazima ma IT wangelifuatilia hili jambo na kubaini hili jambo undani wake....ila kibongobongo ma IT wetu ni mafundi simu na mawinga tu.
Ishu sio Ma IT, ishu ni mfumo.

Mfumo wetu wetu hauna uwajibikaji kitu ambacho kinatia uvivu kufanya hata ufuatiliaji wa huu wizi ambao makampuni wanatuibia.

Unakuta hisa zaidi ya 30% ya hilo kampuni zinamilikiwa na mwanasiasa mkubwa mwenye nguvu.

Na mahakama zetu unazijua, simu moja tu inaweza kubadilisha muelekeo mzima wa kesi.

Au wakijua hali yako ya kiuchumi ni ndogo wanaweza ku play delaying trick, kesi ikawa inahairishwa kila siku utaishiwa resources zako mwisho kesi inafutwa.
 
Airtel ******* sana, nilinunua router kwa 100k ODU wakanambia baada ya hapo ntanunua ya 70k. Duuuh baada ya bundle kuisha wananiambia hawana bundle ya 70 sijui chapakazi. Nikalivunja li odu nikabaki na powerbank tu
 
GB400 kwa mimi peke yangu sizimalizi hata kama tukiwa wawili.

ila Unlimited nnavyojua ina maana bila kikomo, sasa kama ina limit maana yake ni uhuni unafanyika. Itawafanya na wengine wasishawishike kwa hilo, mitandao ya bongo miyeyusho tu.
 
Sasa inasemekana hadi kwenye Fiber ya TTCL mwezi huu wameanza FUP, kuna watu wameanza kulia huko..
 
Kila alichokitengeneza mwanadamu kina speed gorvernor. Gari ina speed 180km kulinda usalama wako, chakula kina kipimo kwenye sahani. So, internet pia ni hivyo hivyo. Kwa hiyo elimu hii ikifikia watu wengi, watajua kuwa wanatembea ndani ya barabara yenye alama, ishara na vijidhibiti mwendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…