Huu ndo upendo bana. . . . !

Huu ndo upendo bana. . . . !

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,891
Unapoamua kumfuga mbwa au paka,anakukubali ulivyo,hata uwe huna mguu mmoja,uwe mweusi,uwe na chongo au uwe huna hela yeye hajui hayo anachojua yeye ni kukupenda tu,hawezi kuhamia nyumba ya jirani na akakudharau kisa jalala la nyumba ya jirani linatupwa minofu!Vivyo hivyo mtoto mchanga hahitaji mama yake awe na gari au awe mweupe au aongee kiingereza ndo ampende,yeye anachojua huyo ni mama haitaji sababu zaidi ya hiyo!Unafki na uchoyo wa binadamu huja kumharibu mtoto huyu na kuanza kuwapima watu kwa muonekano wa nje!Ujinga huu huendelea mpaka kwenye kuchagua wenza wa maisha.Tunachaguana kwa mtazamo wa mali,rangi,sura n.k,sio ajabu kusikia nataka mke/mume awe sijui mweupe,sijui kazi fulani yakimshinda anawehuka.Hatujui upendo ndo msingi wa furaha!
 
kwenye mstar wa mwisho, macho yamenisimama
 
Eiyer, yaani mie leo nimejikuta nalalamika wakati wanaopendana wengine.

Nilikuwa salon ya mabinti, kuna kakijana huwa kanapaka pale rangi.

Mara akaingia binti mzuri nikajikuta nimetoa tabasamu, mara naskia wale wadada wanamwita wifi.
Nikajiuliza wifi kwa nani? Kumbe ni mpenzi wa yule mpaka rangi na amekuja kuleta malalamiko yule kijana kapata jimama jipya.

Yule kijana akaanza kujitetea lakini ilivyoonekana kuna ukweli, basi ili amsamehe akamwambia amwongezee pesa ya kutengeneza nywele 3500, yule kijana hana.

Akalalamika weee yule binti hela huna, majimama huyaachi basi tabu tupu. Baada ya purukushani kama ya nusu saa, hao wakaanza kucheka pamoja kama vile hakuna lililotokea.

Ukimwangalia binti, yule kijana labda awe mjakazi wake, kuna tuvijana tunachagua kondoo walonona afu wanapendwa vile vile.
 
EIYER pole, kuna mtu anakutetea apertheid au assimilation policy karne hii?? pole mwaya!
 
Kongosho,umenikumbusha story ya dada mmoja ana duka mule nssf(nyumbani hotel)halafu anatumiwa na dogo mmoja mpiga debe wa hiace,yule dogo anampeleka puta yule dada wa watu we acha tu.Wakati mwingine sio kupenda ni maradhi ya kisaikolojia!
 
Eiyer, please don't mix conditional and unconditional love. Nitampenda mama yangu regardless kwasababu ni unconditional love, lakini mpenzi ni lazima niweke vigezo na hivyo vigezo ndio inakuwa ni conditional kwasababu vitu kama physical attraction and satisfaction involved kwahiyo I have to match my needs at the end you can't compare the two!
 
Last edited by a moderator:
Eiyer, umenivuta kwenye malezi ya watoto. Kuna watoto wanamkubali kila mtu anayeingia kwao regardless of hali yake ya kiuchumi, kimuonekano etc. Na wanakuzwa hivyo na wanaendelea na mtazamo huo huo.

Bible inasema 'mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapokuwa mzee'. Upendo na jinsi ya kupenda mtu hufundishwa toka utotoni.
 
Eiyer, please don't mix conditional and unconditional love. Nitampenda mama yangu regardless kwasababu ni unconditional love, lakini mpenzi ni lazima niweke vigezo na hivyo vigezo ndio inakuwa ni conditional kwasababu vitu kama physical attraction and satisfaction involved kwahiyo I have to match my needs at the end you can't compare the two!

Listen madame,ukishaweka masharti huo sio upendo,vitu vinavyoonekana havina mashiko,hebu mkubali kila mtu kwa ubinadamu wake uonje utamu wa furaha!(najua hujauonja)
 
Last edited by a moderator:
Yes King'asti,kama ilivyo kwenye uimara wa nyuma ni msingi,kwa mtoto malezi ni nguzo na chimbuko la mtazamo wa mtoto maisha yake yote!Lakini upendo wa kweli aliozaliwa nao mtoto kabla halishwa uchafu wa wanadamu huonekana utotoni!Hata mama yake awe vipi atamlilia tu!Sweet love!
 
Unapoamua kumfuga mbwa au paka,anakukubali ulivyo,hata uwe huna mguu mmoja,uwe mweusi,uwe na chongo au uwe huna hela yeye hajui hayo anachojua yeye ni kukupenda tu,hawezi kuhamia nyumba ya jirani na akakudharau kisa jalala la nyumba ya jirani linatupwa minofu!Vivyo hivyo mtoto mchanga hahitaji mama yake awe na gari au awe mweupe au aongee kiingereza ndo ampende,yeye anachojua huyo ni mama haitaji sababu zaidi ya hiyo!Unafki na uchoyo wa binadamu huja kumharibu mtoto huyu na kuanza kuwapima watu kwa muonekano wa nje!Ujinga huu huendelea mpaka kwenye kuchagua wenza wa maisha.Tunachaguana kwa mtazamo wa mali,rangi,sura n.k,sio ajabu kusikia nataka mke/mume awe sijui mweupe,sijui kazi fulani yakimshinda anawehuka.Hatujui upendo ndo msingi wa furaha!

Unapoamua kumfuga mbwa.....
Mwanadamu alipoumbwa na Mungu alipewa utashi tofauti na wanyama, alipewa akili ya kujua mema na mabaya na zaidi alipewa uwezo wa kumiliki na kuamua hatma ya wanyama wengine. Suala la kufuga mnyama ni njia mojawapo ya kutekeleza agizo toka kwa mola. Ima faima lazima wanyama wawe watiifu kwa mabwana zao maana ndio asili ya kiikolojia ilivyo. Hivyo kufuga ama kufungwa si alama ya upendo bali ni alama ya kuonesha mwanadamu amepewa kumiliki na wanyama kumilikwa.
Tunachaguana kwa mtazamo....
....sio ajabu kusikia nataka mke/mume....
Maana halisi ya neno kuchagua ni kama hivyo ulivyoainisha, kwamba vigezo lazima vizingatiwe hii imekuwepo vizazi hata vizazi. Ndio maana hata Adam wa kwanza alipoletewa msaidizi ambaye ni Hawa haikuja kwa muujiza tu bali utakubaliana na mimi kwamba Adam ali"wish" kwanza kwamba afanyiwe msaidizi. Na hata alipomuona huyo mwanamke alimkubali kwa kuwa alikidhi "wishes" zake.
Huwezi kuchagua kama haujataka, vivyo hivyo hauwezi kupanga kama hautaki kuchagua.

Mwisho, kuna vitu tunafanya si kwa kuwa tunataka bali ni kwa ajili ya kutimiza matakwa ya kiasili "nature", ambapo huo upendo u ndani yake.
 
Huwezi tu kumpenda yeyote bana, unless kama kupenda ni voluntary of which I am sure it is not. Of coz ni vizuri ukajitahidi kuheshimu na kutochukia watu bila sababu. Case closed.
 
Back
Top Bottom