Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Unapoamua kumfuga mbwa au paka,anakukubali ulivyo,hata uwe huna mguu mmoja,uwe mweusi,uwe na chongo au uwe huna hela yeye hajui hayo anachojua yeye ni kukupenda tu,hawezi kuhamia nyumba ya jirani na akakudharau kisa jalala la nyumba ya jirani linatupwa minofu!Vivyo hivyo mtoto mchanga hahitaji mama yake awe na gari au awe mweupe au aongee kiingereza ndo ampende,yeye anachojua huyo ni mama haitaji sababu zaidi ya hiyo!Unafki na uchoyo wa binadamu huja kumharibu mtoto huyu na kuanza kuwapima watu kwa muonekano wa nje!Ujinga huu huendelea mpaka kwenye kuchagua wenza wa maisha.Tunachaguana kwa mtazamo wa mali,rangi,sura n.k,sio ajabu kusikia nataka mke/mume awe sijui mweupe,sijui kazi fulani yakimshinda anawehuka.Hatujui upendo ndo msingi wa furaha!