Huu ni kweli kuhusu Kamari

tafsir yako ni hatar sana kwa afya ya binadam,anyway maisha ni kuchagua kk!!!
 
Ungekua na akili hayo madhara unayosema ungetafuta solution yake, biashara zote duniani ni kamari, unaenda kununua nguo dubai mfano, elfu 10 unakuja kuuza elfu 15 bila kujua nani atanunua hiyo nguo. Ukome kuponda ajira za wenzako kwa kusingizia biblia na Quran, Juzi nimetoka kushinda milioni 2 kwa elfu 50 na kodi imekatwa imeenda kwenye elimu bure ya watoto wako, afu umekunywa togwa asubuhi unatukana ajira zinazosomesha hadi watoto wako, Pumbavu sana wewe...
 
Vp sis tunaondesha maisha yetu kwa KAMARI
usitake wote tufanane na hiz dini tuliletewa tu
 
umeongea vema ila hapo kwenye tusi la PUMBAVU naona likikirudia wewe itapendeza zaidi!!!!
 
Tatizo michezo yote ambayo ilikuwa ni burudani imegeuka kuwa biashara ama kamari. Kuanzia hii michezo ya kawaida kama pool table,drwaft, karata bao nk watu wanashindana kwa madau.

Kwenye soka huko ndio biashara kubwa kabisa haswa kwenye haya makampuni ya betting. Wapenzi wa soka nao wamechukulia kama fursa ya kujipatia kipato. Ila ukiwa makini na ukacheza kwa nidhamu nakuhakikishia unapata pesa kibao huku shughuli zako zikiendelea.

Kamari mbaya ni ile inayopoteza muda mwingi ukiwa sehemu moja ama ukicheza ama ukiangalia wenzio wakicheza.

Ila kamari kuna wakati mwingine inalipa.
 

Unacheza kamari lakini hujui madhara yake___subiri siku utakapotiwa kwa mwanandani utakumbuka nasaha/ mawaidha ya mleta uzi___utajuta juto la kuzaliwa. Siku hiyo hakuna cha james wa Abdala atakaye kuja kukuokoa,,,
 
Mmehamia na huku tena, mliochafua viunga vya airport kwa kukata gogo hovyo, huku mkitaka kwenda Israel bila nauli[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Hamna kitu unajua wewe. Kwa taarifa yako kucheza kamari siyo dhambi. Kila kitu ni jinsi unavyokichukulia wewe binafsi. Wanaocheza Kamari huweka pesa kwenye mchezo kwa hiari yao kabisa na tena wanalipa na kodi ya Serikali. Kamari ninayozungumzia mimi ni ile iliyoruhusiwa kisheria. Kama hujaiba, hujadhulumu, hujaua mtu, umetumia pesa yako ya halali kucheza kamari kuna ubaya gani?
Labda nikuulize, hivi ukilima shamba na ukagharamia maelfu ya fedha kuanzia kuandaa shamba, kununua mbegu na kupanda halafu mvua zisinyeshe na mazao yakakauka shambani au ukavuna kidogo sana na kupata hasara; hiyo inatofauti gani na kucheza kamari?
Au ukawekeza pesa zako kwenye soko la hisa (stock market) na mwisho wa siku ukaambulia hasara, hiyo nayo inatofauti gani na kamari?
Au ukaamua kufuga kuku na ukawekeza mamilioni kwa kujenga banda na kununua vifaranga na chakula chao, halafu kuku wote wakaugua "mafua" ya ndege na kufa, hiyo nayo inatofauti gani na kamari?

Kila kitu kina madhara yake na faida zake. Ni namna tu unavyofanya. Mimi naamini kuwa kila kitu kikifanyika kwa kiasi na kwa utaratibu basi hakina madhara. Kuna namna ya kucheza kamari na ukafanikiwa sana tu na pia kuna namna ukicheza kamari unafilisika kabisa. Pia kuna namna ya kuwa mkulima mzuri na ukafanikiwa, lakini pia ukiwa mkulima "mjinga" unafilisika na kuwa maskini vile vile. Hata biashara pia ni hivyo hivyo. Wapo wengi tu wamefanya biashara na kuishia kufilisika kabisa na kubakia na majuto. Na kuna watu wanacheza kamari na wanapiga "hela" ndefu kila siku.

Kwa kifupi, chochote unachokifanya, kifanye kwa akili na maarifa na kiasi. Ndiyo maana hakuna mahali ukisoma kwenye Biblia utaona imeandikwa usicheze kamari. Lakini imeandikwa "kuweni na kiasi katika mambo yote". Dhambi ni nini? Dhambi ni kuasi, kwa kuvunja amri, sheria na maagizo ya MUNGU. Biblia haisemi kama kucheza "kamari" ni kuvunja "amri", "sheria" au "maagizo" ya MUNGU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…