Huu ni mmea mdogo lakini wenye mambo makubwa

Huu ni mmea mdogo lakini wenye mambo makubwa

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Mmea Mdogo Wenye Mambo Makubwa: Utumie kama chakula dawa ili uepuke kutumia dawa kama chakula!* KIVUMBASI

1. Huu mmea umesambaa Afrika nzima kwa majina tofauti:

Kanda ya Ziwa unaitwa Lumbalumba,
Nyanda za Juu Kusini wanauita Mnunganunga, Kilimanjaro wanauita Mnyenye,
Tanga ni Luvumbampuku,
Wahaya na Wanyambo wanauita Kashwagara, Kenya ni Kivumbani,
Uganda Mjajanuka,
Burundi agacaruzo,
Kongo Tolumbalumba,
Malawi Kavavumba,
Comoro wanauita Nkadi
na wengine wanauita Mwinula yaani uinuliwe.

2. Tumia huu mmea kama chai kila siku, au tafuna tu majani yake, au weka hata kwenye mboga, gonga, faida zake ni nyingi!

3. Wasukuma wanauitumia kutibu chango za watoto wadogo. Wanyambo hutumia kutibu tumbo linalovuruga na kuuma mara kwa mara).

4. Wazee ukiwa unatumia huu mmea kama kinywaji utasahau homa zote, mafua yote.

5. Ni mmea wenye nguvu ya kimungu. Wahindi na Bara la Asia wameupa heshima kubwa.

6. Wanauita Sacred plant (Mmea Mtakatifu), Mother Medicine of Nature (Mama wa Dawa za Asili), The Queen of Herbs (Malkia wa Mitishamba), The Incomparable One (Hakuna Mmea wa Kuulinganisha Nao).

7. Mmea huu ni tiba ya kifua, kata majani yake, tafuna. Unavidonda vya koo? Chukua majani yake, chemsha, sukutua imeisha.

9. Unastress, unaonekana kuchanganyikiwa, chukua majani hata 15, tafuna utarelax.

10. Kwa matatizo ya meno, harufu mbaya ya kinywa na fizi kutoa damu, kausha majani yake, twanga, tumia unga kupigia mswaki.

11. Una mafua makali? Chuma majani yake, yafikiche, weka puani baada ya dk 15 utapiga chafya sana, mafua kwaheri.

12. Ni dawa nzuri ya kufukuza mbu. Ng’oa nzima nzima na mizizi yake, weka ndani, mbu wanakimbia. Au pia choma majani yake kwenye moto, mbu kwaheri.

13. Kiboko ni hii hapa, chukua majani ya kivumbasi, weka kwenye ndoo ya maji, fikinya humo, oga, mwili unakaa sawa..

14. Muogeshe hata mwanao kabla ya kulala uone usingizi mtamu atakaopata. Jifukize pia utaona maajabu yake.

15. Maumivu ya hedhi, hedhi haitoki kwa wakati na ikitoka inatoka kwa muda mrefu? Chukua majani yake, fikicha kwenye maji, hakikisha maji yanadilika rangi, kunywa mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu kisha leta ushuhuda mbuzi nile.

16. Tiba Ya Miguu Kuwaka Moto
Chukua majani ya mti wa Mvumbasi, unguza pamoja na majani ya mti wa mnungunungu, halafu changanya na mafuta ya taa lita moja. Matumizi: Utakuwa unatumia kujichua kwenye miguu kutwa mara tatu kwa muda wa siku thelathini.

17. Lakini pia Wazee wanasema ni dawa nzuri sana ya kuondoa gesi tumboni.

18. Kama vipi, fanya kivumbasi kuwa chai yako ya kila siku, au hata juisi. Hakuna hasara. Faida ni nyingi.

19 . Hutumika kwa magonjwa ya ini, moyo na mishipa ya damu. Huua virusi vya hepatitis vyote.

20 Kwa mtu anayesumbuliwa na tumbo la hedhi upate unga wa majani tumia kwenye maji moto ni tiba nzuri mara mbili kwa siku

21. Hutibu ugonjwa wa red eye Chemsha mvumbasi changanya na majani ya mbaazi hadi maji yawe ya kijani, acha ya poe baada ya hapo nawia uso kutwa mara tatu kwa siku tatu utakaa poa

22. Kwa wanaume Chukua majani ya mvumbasi +mchai chai + Tangawizi (kata vipande) + mdalasini .. Chemsha huo mchanganyiko na ndio iwe chai yako daima usiweke sukari , Msumari wako utasoma namba.

23 . Tiba kwa mtu aliyeingiwa utomvu wa minyaa chukua mbegu zake ukipikicha na kuziweka machoni .. utomvu wote wa mnyaa utakusanywa na kutolewa nje ya macho

24. Pia kama wewe ni mfugaji wa nyuki basi mmea huu hutumika kuhamishia nyuki kupeleka sehemu nyingine unayoitaka wewe

25. Pia kama unaishi mazingira yenye mbu tumia huu mmea kufagilia uwanja , Mbu wataondoka wote , au kata mmea weka dirishani , Aisee mbu na harufu ya mmea huu n maadui sana .. utalala unono

26. Kama wewe ni Mtalamu wa Kujamba sana, tumbo kujaa gesi tumia mmea huo chemsha kunywa glas moja mara mbili kwa siku

27. Tiba ya wagonjwa wa degedege

28. Kama Unajisikia homa chuma mmea huo , Chemsha kunywa mara mbili na kuogea utapona kabisa

29. Kama unasumbuliwa na vidonda vya koo, macho, kichwa, mafua, kifua, figo chukua majani tengeneza juice kunywa glasi moja asub na Jion

30. kama kuna kuku wanaumwa umwa sana we chukua ayo majani na miti yake fanya kama fagio na ufagie mahala wanapo lala, Angalizo kuku wa mienyeji sio hawa wa kizungu .

31. Kama una shida ya kupumua tafuta huu mmea kisha safisha chemsha kunywa mara mbili kwa siku kwa mda wa siku 14.

32. una pressure ya juu chumua mmea mzima chemsha kunywa mara mbili kwa siku 14 hadi 21 nenda kapume.

33Kama unataka kutunza ngozi yako basi majani yake yafanye yawe ndio majan y chai yako kila siku

ZIPO FAIDA NYINGI SANA KATIKA MMEA HUU NDIO MAANA HUITWA HOLY BASIL (Mmea Mtakatifu).

Ngoja Nimalizie

34. mbengu zake ni dawa nzuri sana ya watu wanaotoka damu puani unachukua unanusa tu hutapata huo ugonjwa tena

35. kama una kikohozi chukua majanj yake na majani ya mbaazi tafuna kwa pamoja siku tatu nyingi

Source: jay orres
 

Attachments

  • Screenshot_20250215_163245.jpg
    Screenshot_20250215_163245.jpg
    540.9 KB · Views: 2
Back
Top Bottom