Huu ni mpira wa kishamba sana

Man Utd walimchukua RVP toka Arsenal akaenda kuwapa ubingwa, Chelsea waliwahi kumchukua Peter Kenyon toka Man Utd kuwa mkurugenzi wao wa ufundi, sidhani wewe ulieanzisha huu uzi kama unaufahamu mpira wa miguu hata kidogo.
 
Kwani kipindi kile anaimbwa Akiwa Yanga alikuwa ametoka nayo wapi? Huu ni wivu wa kike. Anavyoimbwa messi huwa wengine hawachezi? Kila mtu na bahati yake... Usiwe na wivu hivyo fanya yako.

Akina Kagere, Boco waliopambania timu sasa ivi wanaonekana takataka, simba wote wanamuimba Morrison usiku na mchana
 
TUNAWACHUKIA KINAFIKI.TATIZO LIPO YANGA....GSM NDO WANAUA MPIRA KWA UHUNI WAO. HAWA JAMAA NI SMART WAMETUZIDI KWA UPUMBAVU WETU.


Hans Pope,Manara na Magori ni kirusi cha Soka la Bongo,na pia sioni usomi na credibility ya MO katika hili amekubali kuendeshwa kama gari bovu na hao Waswahili.
 
Sisi.yanga tunaanzisha nyuzi nyingi za kulia lia badala ya kukemea viongozi wetu wahuni.... Ushamba tunao sisi na morrison ni mtoto wa mjini.

 
Ujinga sana, badala ya kufikiria kupambana na TP Mazembe, Al ahly, Zamalek, wanaishia kulumbana tu, timu zimejaa ujinga ujinga tu
Kama Yanga walivokua wakimuimba na Kumtukuza Morrison baada ya 08 March
 
Unadhan ni Senzo tu alianza kujiuzulu akawa hana pa kwenda ndo Yanga wakamchukua

Au

Walishakubaliana na Yanga kabla hajajiuzulu hivyo kujiuzulu kwake ndio njia ya kwenda Yanga?
 
Akina Kagere, Boco waliopambania timu sasa ivi wanaonekana takataka, simba wote wanamuimba Morrison usiku na mchana
kwahiyo ushamba wa akina bocco upo wap?? hamjijui kama nyie ndo washamba??? mashabiki wote wa man united saiv wanamtaja sancho huo nao ni ushamba??? fikilini kabla ya kukosoa au mnahisi wachezaji waliopo simba hawapendwi bac morrison anapendwa sanaa?? Sio hivyo ila ni kama tajili tu anapesa kibao ila anataman kile ambacho hana [emoji23][emoji23]
 
Hans Pope,Manara na Magori ni kirusi cha Soka la Bongo,na pia sioni usomi na credibility ya MO katika hili amekubali kuendeshwa kama gari bovu na hao Waswahili.
Tukubaliane kwanza morrison ni mchezaji mbovu??? pili simba na yanga wangekaa mezani biashara ya morrison ingefanyika?? usihukumu kitu bila kukiangalia kwa pande zote
 
Ujinga sana, badala ya kufikiria kupambana na TP Mazembe, Al ahly, Zamalek, wanaishia kulumbana tu, timu zimejaa ujinga ujinga tu
Cha ajabu hao walioshauri timu ziendeshwe kprofessional kama MO ndo wanaofanya upuuz
 
Hayo ni mawazo yako.Swala la mchezaji kuhama timu moja kwenda nyingine ni kawaida, swala la uhasimu mnalijua nyie mashabiki ila kwa mchezaji kwake ni ajira na maisha na kwa viongozi kwao ni maslahi ya timu nayao binafsi.Na lazima ujue timu inachukua mchezaji kutokana na mahitaji na kiwango cha mchezaji kwa wakati huo lakini pia na uwezo wakifedha.Kinachofanyika sio kigeni kwenye ulimwengu wa soka, Tatizo linakuja pale tusipofanya mambo kwakufuata utaratibu na utulivu.Sasa hilo ni tatizo la nchi na jamii nzima.Mambo mengi tunayafanya kwa papara na mihemko ndo maana matokeo yake yanakua na tatizo.Swala la Morison limetengenezwa na Yanga wenyewe likakuzwa na simba.Nahiyo yote nikwasababu yakukosa utulivu wa viongozi wahivyo vilabu.
 
Msitoe hoja kimihemuko bila facts waziri mwakyembe hawezi kuzuia usajili wowote ukiwa tu ni halali na hauvunji sheria yoyote
Kitu kingine si kweli kwamba simba inafanya usajili kwa lengo la kuikomoa yanga simba inafanya usajili kulingana na wachezaji inawahitaji kwa wakati huo
Suala la mchezaji kusajiliwa na simba na kukaa benchi wala sio point ya msingi,ukiachana na Gadiel,Ajibu na Beno ambao wametoka yanga na wanakaa benchi pia kuna Shiboub toka sudan nae anakaa benchi hata Deo kanda pia toka congo hana uhakika wa namba kwahiyo simba hao pia aliwassjili kwa lengo la kuvikomoa vilabu vyao?
Suala la mchezaji kusajiliwa ni moja suala la kupata namba ni jingine mfano Gadiel amesajiliwa akiwa ni mchezaji bora kabisa katika walinzi wa pembeni pengine wakati yupo yanga ilikuwa ni ngumu kupata jibu la moja kwa moja nani bora kati yake na Tshabalala na hata timu ya taifa mara nyingi tu Gadiel alikua akianza mbele ya Tshabalala sasa inakuwaje ni kuikomoa Yanga endapo simba itaamua kumuongeza mtu wa kiwango hicho klabuni ili kuongeza ushindani na kuwa na options mbili zenye uwezo unaoelekeana katika nafasi ya beki wa kushoto? Je kuna haja ya kumzungumzia Ajibu alivyokuwa kabla ya kuja simba? Kwahiyo hao wote kukaa benchi imekuja kutokea tu kama ilivyo kwa shiboub na wengne wanaokaa benchi lakini hawatokei yanga
Kuhusu usajili wa Morrison nawapa pongezi viongozi wa simba watu labda hawaelewi mchezaji mzuri wa kiwango cha morrison kwa sasa ukimkuta kwa wenzetu sio rahisi kumng'oa kwa pesa za madafu uliza simba wamelipa kiasi gani kwa Miquissone? Sasa simba wanaachaje kumchukua BM ambaye yupo free na dau lake ni la kawaida ukilinganisha ubora wake eti tu kisa aliwahi kuwa yanga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…