monde arabe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2017
- 8,781
- 13,444
Husikeni na kichwa cha habar ndugu wasomaji.
Umewadia muda ambao Taifa la Tanzania linahitaji Katiba mpya na hapa ndipo ambapo kila mmoja anapaswa kuonyesha uzalendo wa kweli.
KWANINI TAIFA LA TANZANIA LINAHITAJI KATIBA MPYA?
Taifa la Tanzania linahitaji Katiba mpya kwa sababu iliyopoina mapungufu mengi sana kuanzia kwenye nyanja ya uchumi,elimu,siasa na afya pia.
Kama Taifa hatuna dira nzuri kwenye uwekezaji (uchumi)
Kwa muwekezaji mwenye akili timamu hawezi kuleta mtaji wake Tanzania kwa kuwa mazingira ya uwekezaji yanategemea ufahamu na utashi wa wanasiasa (watawala) ambao kimsingi hawafahamu lolote kuhusu uchumi.Muwekezaji anaweza kuwekeza mtaji wake Tanzania na baada ya mwezi mmoja mwanasiasa au mtawala anatengeneza sera mpya ambayo ni hatar kwa muwekezaji mfano kupandisha kodi na kuweka urasimu mwingi usiokuwa na tija kama alivyokuwa akifanya Magufuli.
Pia,kwenye elimu, siasa, ulinzi na afya napo bado kuna madudu mengi sana.Hakuna sera bayana zaidi ya kutegemea utashi wa wanasiasa. Kumbukeni kwenye uchaguzi wa mwaka 2019 na 2021. Kumbukeni kuhusu Issue ya Corvid-19 kwa hapa kwetu Tanzania. Kumbukeni issue ya tetemeko la Ardhi Bukoba (Kagera) Mh.Rais wa kipnd hicho ndugu John Magufuli alisema "tetemeko halikuletwa na serikali so, siwezi kutoa chakula" lkn,muda huohuo alitoa chakula na madawa kwa waathirika wa mafuriko kwa nchi jirani.
Kwa kifupi ni tunaishi kwenye Taifa ambalo hakuna mtu aliyesalama kutokana na aina ya katiba tuliyonayo.
Tunahitaji katiba mpya kwa kuwa ni hitaji la Taifa kwa nyakati tulizonazo na kama tutaendelea kupuuzia jambo hili tutegemee kuishuhudia hatar kubwa sana kuliko hatari yoyote iliyowahi kutokea.
Upo mwaka usiojulikana atapatikana mtawala kwa njia za panya kama alivyopatikana Magufuli na wabunge wake na kikundi hicho kitakuja kuua watu wengi ikiwa ni pamoja na kuharibu biashara za watu na mfumo wa maisha kwa ujumla.
Katiba mpya ndiyo dira na uelekeo wa wapi Taifa linaelekea.Tuungane wote kuhakikisha kuwa Taifa linapata Katiba mpya.