Huu ni mwaka wa hasara kwa wakulima

mkulu senkondo

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
1,862
Reaction score
3,574
Hali ni mbaya sana!

Licha ya uchumi wa watanzania wengi kutegemea kilimo cha kutegemea neema za Mwenyezi Mungu kupata riziki zao lakini bado hali ya masoko imekuwa mbovu sana.

Katika hali ya kusikitisha sana mwaka huu sio mzuri sana kwenye mavuno hivyo uwezekano wa waliowekeza kwenye kilimo kupata hasara upo kwa kiasi kikubwa.

Mbaya zaidi hali ya upatikanaji wa masoko imekuwa mbovu zaidi kuwahi kurekodiwa katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita.

Kuna baadhi ya watu watakuja hapa kuona kwamba hiyo ni hali nzuri kwao kuona kwamba mazao ya chakula na biashara hayana bei lakini wasisahau kuwa kilimo kinatumia mitaji na kama kinatumia mitaji maana yake ni sehemu ya uwekezaji. Mfano kwa sasa gunia la mahindi halizidi tsh.25000/= katika maeneo mengi nchini hususan maeneo ya vijijini, pia gunia la maharage halizidi 120000/= katika maeneo mengi ya vijijini yanapolimwa. Bado hatujui hali ya mbaazi na mazao mengine katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini.

Je, watanzania wenzangu nini kifanyike ili angalau kuwezesha sisi wakulima tuweze kujifuta machozi kwa mwaka huu? Maoni yenu kwenye jukwaa hili ni ya muhimu sana kwani kwa zaidi ya 80% ya watanzania huwa wanategemea kilimo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili linapaswa lijadiliwe kwa kina
Blogger & Trainer
 
Msimu huu nimegundua aheri kwa mahindi usage unga si haba, kwa mara ya kwanza toka nilipoanza kulima mahindi miaka mitano iliyopita nimethubutu kusaga dona, sembe, bada na dona lililochanganywa na bada (makopa) na kupack na ninauza tena kwa order, yaani nikishakusanya order za wateja ndio napeleka mahindi mashineni.

Kikubwa ni kuongeza thamani ya mazao tunayoyazalisha japo nikimfikiria yule mkulima mwenzangu kule kijijini ni ngumu sana kuweza kuongeza thamani ya mazao yake.

Pia tuepuke kulima mazao yaliyozoeleka mfano mahindi yanalimwa na wakulima kwa asilimia kubwa, sasa kwanini tusilime mazao mbadala? Pia itasaidia kupumzisha ardhi kurudia kulima zao hilohilo kila msimu.
Nawazaga kama issue ni kupata chakula kwanini usilime mfano, alizeti au ufuta kisha ukiuza mavuno yako ukanunua chakula kuna tatizo gani?

Ila yote kwa yote hiki kilimo cha kutegemea mvua ni mwendo wa kubahatisha tuu lakini tutafanyaje wakti kuyapata maji katika mashamba yaliyopo mbali na water bodies ni gharama kubwa mno.
 
Kwa hiki kinacho endelea Tutegemee upungufu mkubwa wa chakula baada ya muda. maana kila mtu atapunguza uwekezaji kwenye hiyo sekta. Kwakweli sekta ya kilimo hasa cha mahindi na mbaazi kama jitihada za maksudi hazita chukuliwa. Basi athari zake tutaziona hivi punde
 
Mnachokosea ni kuleta mamisamiati yenu ya kisiasa kwenye uti wa mgongo wa uchumi wa nchi.
Mara uwekezaji, eti mara sekta!! Yaani full maneno eti ya kitaalamu kwenye jukwaa la kisiasa.
Mkishashiba kilimo mnakitukana, utasikia "mshamba wewe" n.k

Hapa hamtafuti suluhisho, mnakusanya taarifa mpate fursa hatimaye muwatukane watu kanakwamba ni washamba.
Najitenga na husda hii.
 
SEKTA na KUWEKEZA Hivi Ni Maneno Ya kisiasa??. Lipi Baya nililo lisema hapo?. Nadhani hizi tuhuma hazikupaswa kuelekezwa kwangu labda kama kuna Issue Nyingine ila si kwa hichi nilichochangia hapa.
 
SEKTA na KUWEKEZA Hivi Ni Maneno Ya kisiasa??. Lipi Baya nililo lisema hapo?. Nadhani hizi tuhuma hazikupaswa kuelekezwa kwangu labda kama kuna Issue Nyingine ila si kwa hichi nilichochangia hapa.
Nimetumia akili inayotukanwa daily (akili ya mkulima i.e mshamba) sidhani kama unaweza kukiona nilichokisema ukakielewa! Unataka nikuelewe tu na si vinginevyo.
 
Well said
Alafu inachosikitisha ni uwongo tu!
Mtu anakaa siku nzima kutafuta uwongo wa kuleta JF kwa sababu ya uvivu!
Pathetic walahi
 
Nimetumia akili inayotukanwa daily (akili ya mkulima i.e mshamba) sidhani kama unaweza kukiona nilichokisema ukakielewa! Unataka nikuelewe tu na si vinginevyo.
Ipi point yako maana naona kama nachangia kitu ambacho sikijui.
 
Well said
Alafu inachosikitisha ni uwongo tu!
Mtu anakaa siku nzima kutafuta uwongo wa kuleta JF kwa sababu ya uvivu!
Pathetic walahi
Uongo ni upi mkuu?! Hapa nilipo mahindi gunia ni Tsh 18,000 baada ya kuongezeka bei kutoka 12,000. Muwe mnaacha kuingiza itikadi kwenye mambo yanayokera wananchi.
 
hapa kuna wabwabwaja mdomo na ambao wapo mashamban wanajua bei za mazao na wanapractice kulima!yangu macho na masikio!tangawizi inaenda kwa shilingi 700 kutoka 3000! mtu mzima unatoka huko na khanga moko unasema mwenzako mvivu na hapo anaongelea facts!mxiew
 
Uongo ni upi mkuu?! Hapa nilipo mahindi gunia ni Tsh 18,000 baada ya kuongezeka bei kutoka 12,000. Muwe mnaacha kuingiza itikadi kwenye mambo yanayokera wananchi.
Mkuu hiyo mkoa gani gunia Tsh 18,000??
 
Kwa mkulima , kwa madalali Sumbawanga mjini ni 30,000/ tangu mwaka jana haipandi wala kuteremka.
Poa poa mkuu. Kwahiyo ni wilaya gani ili nijue hiyo sehemu siku nikija nisipate shida?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…