mkulu senkondo
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 1,862
- 3,574
Hali ni mbaya sana!
Licha ya uchumi wa watanzania wengi kutegemea kilimo cha kutegemea neema za Mwenyezi Mungu kupata riziki zao lakini bado hali ya masoko imekuwa mbovu sana.
Katika hali ya kusikitisha sana mwaka huu sio mzuri sana kwenye mavuno hivyo uwezekano wa waliowekeza kwenye kilimo kupata hasara upo kwa kiasi kikubwa.
Mbaya zaidi hali ya upatikanaji wa masoko imekuwa mbovu zaidi kuwahi kurekodiwa katika kipindi cha mwongo mmoja uliopita.
Kuna baadhi ya watu watakuja hapa kuona kwamba hiyo ni hali nzuri kwao kuona kwamba mazao ya chakula na biashara hayana bei lakini wasisahau kuwa kilimo kinatumia mitaji na kama kinatumia mitaji maana yake ni sehemu ya uwekezaji. Mfano kwa sasa gunia la mahindi halizidi tsh.25000/= katika maeneo mengi nchini hususan maeneo ya vijijini, pia gunia la maharage halizidi 120000/= katika maeneo mengi ya vijijini yanapolimwa. Bado hatujui hali ya mbaazi na mazao mengine katika maeneo tofauti tofauti hapa nchini.
Je, watanzania wenzangu nini kifanyike ili angalau kuwezesha sisi wakulima tuweze kujifuta machozi kwa mwaka huu? Maoni yenu kwenye jukwaa hili ni ya muhimu sana kwani kwa zaidi ya 80% ya watanzania huwa wanategemea kilimo.
Sent using Jamii Forums mobile app