Huu ni mwaka wangu wa mwisho kuajiriwa

Kabla hujaacha kazi,jiulize je una plan b?ikitokea mradi haujafanikiwa utafanya nini ili kuitimizia familia mahitaji yake daily?mana kuna magonjwa,kula nk!
Ukiwa na hiyo plan b acha uende,ila kama huna usiache hiyo kazi!
 
Mkuu hakuna uwezekano ukafanya uwekezaji mahali huku ukiendelea na kazi nyingine?
 
Kabla hujaacha kazi,jiulize je una plan b?ikitokea mradi haujafanikiwa utafanya nini ili kuitimizia familia mahitaji yake daily?mana kuna magonjwa,kula nk!
Ukiwa na hiyo plan b acha uende,ila kama huna usiache hiyo kazi!
Plan b ipo,nimeandika kuwa nitamfungulia wife biashara pale nyumbani maana kuna nafasi ya kufanya hivyo..
 
Mkuu hakuna uwezekano ukafanya uwekezaji mahali huku ukiendelea na kazi nyingine?
Shida ni capital mkuu,mshahara unaishia kwenye matumizi nyumbani tu, na mda mwingine changamoto zinazidi kipato.
 
fanya hivi chukua milioni mbili au nne njo mafia kodi boti ndogo au jahazi jahazi unaweza nunua jahazi itakuwa inasafirisha mizigo au ukikodi boti na nyavu itakusaidia kuvua samak huku kukodi sawa na laki nane miezi minne au sita hio pesa unaweza irudisha kwa siku tatu au mbili uvuvi ukikubali
 
Karibu sana mtaani. Wazungu wanasema it is easier said than done. Sijajua umehesabu miaka mingapi hapo maana ulivyoelezea ni kama kila kitu ni Mtelezo sana.

Pitia hii video itakusaidia

 
Fuata ndoto zako na nafsi yako inavyokutuma .

Usiwasikilizs walimwengu.

Amini unachokitaka na fuata unachoamini .

Ajira zinachosha sometime hasa Kama maslahi Ni duni kazi nyingi muda huna ,watu wale wale hawakupi changamoto.



Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Ujasiriamali ni mgumu na ni utumwa kuliko ajira hasa hatua za mwanzoni.

Usiache kazi kuingia kwenye kilimo, ingia kwenye kilimo wakati bado una kazi.

That being said, lazima uchukue risks kufikia malengo yako but they got to be calculated risks. Good luck
 
Hizi ndio akili,leta mrejesho mambo yatakavyokuwa huko shambani,unaweza ukawa nabii mzuri na wengine tukafuata mfano.
Hizi ajira huwa tunazikimbilia kwa vile hakuna mbadala,lakini mifumo ya kujiajiri ingekuwa rafiki,nani anataka kupata taabu ya kusimama kutoka mbezi mpaka posta,unaenda kazini,na kurudi hivyo hivyo mwisho wa mwezi unakula Laki sita,hukopesheki,uwezi kununua shamba,huwezi kujenga kabla hujafika 40s
 
All the best..
Asilimia kubwa ya watu hata walioajiriwa at one point watastaafu na kulazimika kujiajiri..
Cha Msingi anza kufanya kwa kupenda(Do it with Passion)..kisha maslahi yafuate.
Ukitanguliza maslahi,mambo yakienda mrama unaweza kata tamaa kabisa ushindwe kunyanyuka..
Usisahau kutupa mrejesho huko mbeleni ili wengine tujifunze..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Mkuu ela za mafao usiziamini kabisa katika kuzipata zote.
Sisi kazi iliisha na tukaja kupewa mafao miezi karibia nane baada ya kukosa ajira na apo tulipewa asilimia chache sana na tukaambiwa zingine baada ya waka kupita.
Usitegemee sana NSSF wanaweza kukuangusha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…